Quantcast
Channel: EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Viewing all 16721 articles
Browse latest View live

RAMBIRAMBI MSIBA WA JAMES KISAKA

0
0


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, James Kisaka (57) kilichotokea leo asubuhi (Desemba 25 mwaka huu) katika Hospitali ya Burhani, Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu kwani Kisaka kabla ya kuwa kocha alikuwa mchezaji katika nafasi ya kipa. Mbali ya Simba, timu nyingine alizowahi kudakia ni Ndovu ya Arusha, Volcano ya Kenya na Small Simba ya Zanzibar.

Akiwa mwanafunzi Shule ya Sekondari Tambaza jijini Dar es Salaam aliwahi kuchezea timu za Oysterbay Stars, Eleven Stars ya Msasani, Sigara wakati ikicheza Ligi ya Temeke na Nyota Nyekundu kabla ya kutua Simba.

Pia alikuwemo kwenye timu ya Taifa ya vijana iliyokwenda Zimbabwe kwenye sherehe za uhuru wan chi hiyo mwaka 1980. Vilevile alikuwa mmoja wa wachezaji waliounda kombaini ya Tanzania ya UMISSETA akiwa na akina Said George, Nico Njohole, George Kulagwa na wengine. Hivyo mchango wake katika mchezo huu tutaukumbuka daima.

Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Benny Kisaka, James alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu kufa ganzi na matatizo ya kutoona vizuri.
R
Msiba uko nyumbani kwake Mbezi Mwisho (Kwa Yusuf), na anatarajia kuzikwa nyumbani kwao Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kisaka, klabu ya Simba na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Marehemu Kisaka ameacha mjane na watoto wanne. Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU SHEIKH SULEIMAN AMOUR JENDELE ZANZIBAR

0
0


 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki kwenye Dua ya pamoja na Familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) kwenye Makaburi alipozikwa kijijini kwake Jendele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kufariji familia hiyo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) aliyefariki Dunia hivi karibuni wakati alipofika nyumbani kwa marehemu katika kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki kwenye Dua ya pamoja na Familia ya marehemu Sheikh Suleiman Amour (82) wakati alipofika nyumbani kwa Marehemu katika kijiji cha Jendele Wilaya ya Kati Unguja kwa ajili ya kufariji familia hiyo leo.Picha na OMR

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

0
0


MAJAMBAZI-8 
“PRESS RELEASE” TAREHE 25.12. 2013.
WILAYA YA MBARALI – AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA  KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI.
MNAMO TAREHE 24.12.2013 MAJIRA YA SAA 17:30HRS HUKO ENEO LA MASHAKA KATA YA IGURUSI TARAFA YA ILONGO WILAYA YA MBARALI MKOA WA  MBEYA. GARI NO. T.843 CKL/T693 CKL AINA NA SCANIA LIKIENDESHWA NA MUGONI S/O LUSENGA, MIAKA 32, MSUKUMA, MKAZI WA DSM ALIGONGANA USO KWA USO NA GARI NO. T830.BQJ AINA YA  T/SALOON  LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE GODFREY S/O BONIFAS, MGANGA MTAFITI MKAZI WA DSM  NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATATU AMBAO BADO HAWAFAHAMIKA  MAJINA YAO WALA ANUANI KATI YAO WANAWAKE WAWILI NA MWANAUME MMOJA WALIOKUWA KATIKA GARI NO. T.830 BQJ T/SALOON NA DEREVA WA GARI HILO AMEJERUHIWA NA KULAZWA KATIKA HOSPITALI YA  CHIMALA MISSION. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA GARI NO. T.830 BQJ KUTAKA KUYAPITA MAGARI YALIYOKO MBELE YAKE. DEREVA WA GARI NO. T.843 CKL/T.693 CKL AINA NA SCANIA AMEKAMATWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI HASA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI. AIDHA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUEPUKA MWENDO KASI KWANI UNAUA NA KUSABABISHA MADHARA MAKUBWA.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 24.12.2013 MAJIRA YA SAA 23:00HRS HUKO AIRPORT, KATA YA IYUNGA, TARAFA YA IYELA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA BONIFACE S/O SAJILE, MIAKA 24, DEREVA NA MKAZI WA IGURUSI AKIWA NA BHANGI KETE NNE SAWA NA UZITO WA GRAM 20. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MARA BAADA YA KUPEKULIWA KWENYE MIFUKO YAKE YA SURUALI. MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI HIYO, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAENDELEA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA TABIA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA WAKULIMA KUACHA KULIMA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJIKITE KATIKA KULIMA MAZAO YA CHAKULA NA BIASHARA.
[B.N.MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MISS TANZANIA 2013 ASHEREHEKEA SIKUKUU YA X – MASS NA WATOTO YATIMA MOROGORO

0
0

 

 
 
 Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa Akikabidhi zawadi waliotoa katika kituo hicho kwa Mama Mkuu wa Wa shirika la Masista wa Moyo safi wa Maria Sista Flora Chuma..
 Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa (pichani), Leo amejumuika na watoto yatima wa kituo cha Mgolole  kilichopo Bigwa nje kidogo ya Mji wa Morogoro. Mrembo huo ameungana na warembo wengine wawili , akiwemo Miss Kanda ya Mashariki Missa Clara Pamoja  Sabra Islam Miss Morogoro 2013 . Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa.Aliongozana na Wazazi wake pamoja na Ndugu jamaa na marafiki zake
  
 Mkurugenzi wa  kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega Akiwa na  Katibu wa Miss Tanzania Bosco Majaliwa leo alipoongozana na Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa Alipotembelea Kituo cha Kulea watoto Yatima cha Mgolole Kinachomilikiwa na Masista wa Moyo safi Wa Maria  Cha Mkoani morogoro
 Watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha masista wa Moyo Mtakatifu wa Maria cha Mgolele mkoani Morogoro wakiwa katika Picha ya Pamoja leo walipopata Ugeni Kutoka kwa Miss tanzania Happiness Watimanywa Aliyeambatana na wakurugenzi wa Miss tanzania Pamoja na Wazazi wake ndugu na jamaa wake wa Karibu.
 Ndugu na Marafiki wa  Miss tanzania 2013 waliomsindikaza Happiness Watimanywa  Alipotembelea kituo cha watoto yatima cha mjini Morogoro..

 Mama na Mwana : Miss Tanzania 2013 Hapiness Watimanywa Kulia akiwa na mama yake mzazi  
 
Wazazi wa Miss Tanzania Bwana na Bibi Watimanywa katika picha pamoja na Mtoto yatima wa Kituo cha Mgolele walipomsindikiza Mtoto wao Ambaye ni miss tanzania 2013 Hapiness Watimanywa alipoenda kusherekea Sikukuu ya Chrismass pamoja na watoto hao leo ambapo amepata mapokezi mazuri kutoka kwa uongozi wa kituo hicho leo
 Miss tanzania 2013 Hapiness Watimanywa Akiwa pamoja na wadogo zake wakiwa wamewabeba watoto katika yatima wa kituo hicho leo
 
 
 
 
CHANZO : MATUKIO BLOG

WANAFUNZI WA CBE DODOMA WATOA MKONO WA KHERI YA KRISMASS KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA- MIYUJI

0
0



 Hii ni nembo ya kituo hiki iyonacho sadifu mazingira harisi ya watoto wanolelewa mahari hapa.
Remidius M. Emmanuel (Rais wa Serikali ya wanafunzi CBE ya Dodoma) akikabidhi zawadi hizi kwa mlezi wa kituo hiki zilizopokelewa na mtoto katika kituo cha Watoto Yatimu cha Miyuji jana tarehe 24/12/2013 mnamo saa tano asubuhi, akitoa pongezi kwa Mlezi wa kituo hicho Sister Glory Shayo kwa kulea watoto hawa. Rais aliwasilisha baadhi ya vitu kwaajili ya watoto hao.Vitu vilivyotolewa ni Mchele kilo 50,Ngano kilo 50,Mafuta kula lita 20,Mafuta ya kujipata  dazan 1 naMaji carton 2.
Mlezi wa kituo hicho Sister Glory Shayo akipoke ndoo mbili za mafuta ya kula
Mtoto anayelelewa kwenye kituo icho akipokea mafuta kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa katika kituo hicho
Huu ndio msaada uliotolewa na uongozi wa Serikali ya wanafunzi CBE ya Dodoma hapo jana
 Rais akiwa na watoto hawa akionyesha upendo kwa watoto Yatima
 Mhe, Remidius M. Emmanuel (Rais wa Serikali ya wanafunzi CBE ya Dodoma) akiwa na baadhi ya viongozi katika kituo cha Watoto Yatimu cha Miyuji jana tarehe 24/12/2013 mnamo saa tano asubuhi, akitoa pongezi kwa Mlezi wa kituo hicho Sister Glory Shayo kwa kulea watoto hawa. Rais aliwasilisha baadhi ya vitu kwaajili ya watoto hao
 "Napenda tuwe mfano mzuri ndani na nje ya chuo, hata Mkoa kuwatembele watoto hawa kujiona nao ni sehemu ya jamii kiujumla" Maneno ya Rais.
Mhe, Yohana akimsikiliza Mhe, Remidius M. Emanuel anavyo toa zawadi hizo
 Watoto hawa wakiongea na ndugu Dominicky Stephano na nyuso zao zikionekana ni za furaha 


 Waziri wa Fulsa na Mipango Mhe, Riziki Shaweji akiwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe, Simba


 Zawadi zilizo tolewa





 Mhe Ignas alipata bahati ya kutembelea shamba la mboga mboga hili ni shamba ambalo kituo kimeweza kuliwekeza kwa ajili ya kilimo hiki cha mboga mboga:


 Hakuna mahari popote duniani panapoweza kuondokana na janga la njaa pasipo kuwekeza katika kilimo vivyo hivyo hivyo katika kituo hiki wameamua kupigana na adui njaa kwa kujiandalia mazao yao: Tazama mashamba haya:

TFF yamtangaza Selestin Mwesigwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho hilo la soka nchini

0
0


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akimtangaza Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho hilo,ambaye ni Selestin Mwesigwa (aliewahi kuwa katibu mkuu wa Yanga) (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Kisheria ya TFF,Wakili Evodius Mtawala (kulia) wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.Kushoto ni Afisa Habari wa TFF,Boniface Wambura.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Kisheria,Wakili Evodius Mtawala nakala ya ilani yake ya uchaguzi wakati akimtambulisha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.kushoto ni Katibu Mkuu wa Mpya wa TFF,Selestin Mwesigwa.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu wa TFF, Selestin Mwesigwa nakala ya ilani yake ya uchaguzi wakati akimtambulisha kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

SHIRIKISHO la soka Tanzania,  TFF limemuajiri Katibu Mkuu wa zamani wa  Timu ya Yanga, Selestin Mwesigwa kuwa katibu mkuu mpya wa shirikisho hilo.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi imesema kuwa, Mwesigwa alizaliwa mwaka 1970,  ana digrii ya masuala ya kimataifa kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam na  diploma ya mafunzo ya sheria.

Malinzi aliongeza kuwa Mwesigwa amefanya kozi kadhaa za masuala ya utawala ndani na nje ya nchi zikiwemo kozi za utawala wa mpira zilizotolewa na FIFA.

 Rais huyo alisema Ajira yake ya  mwisho  ya Mwesigwa ilikuwa Ukatibu mkuu wa klabu ya Yanga ya Dar es salaam, hivyo ana uzoefu mkubwa wa masuala ya uongozi ikizingatiwa amefanya kazi katika mashirika mbalimbali ikiwemo Plan International.

Aidha, Malinzi alisisitiza kuwa Mwesigwa alipokuwa katibu mkuu wa Yanga alishiriki kikamilifu katika mchakato wa kuanzisha Bodi ya Ligi kuu na ule wa Yanga kuingia udhamini na kampuni ya bia ya TBL, hivyo amekidhi vigezo vya kushika wadhifa huo mkubwa ndani ya TFF.

TFF pia imemuajiri katibu wa Simba SC, Wakili Evodius Mtawala kuwa Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Kisheria ya TFF.
Rais Malinzi alisema Mtawala  ana Shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  na Shahada ya Uzamili ya uongozi wa Biashara ya Chuo Kikuu cha ESAMI.

Rais aliongeza kuwa  Mtawala ambaye ajira yake ya mwisho ilikuwa Ukatibu mkuu wa Simba Sc , Klabu mwanachama wa TFF, ana uzoefu ambao utasaidia sana kukabili changamoto mbalimbali za vyama wanachama wa TFF.

Aidha Rais alisema uzoefu wake na ujuzi wa masuala ya sheria utasaidia kutatua masuala mbalimbali ya kisheria na kikatiba ndani ya shirikisho hilo.

Nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF imeachwa wazi kufuatia waombaji wote walioomba wa ndani na nje ya nchi kutokidhi vigezo, hivyo kamati ya utendaji imeagiza nafasi hii itangazwe upya na wale walioomba mara ya kwanza wasiombe tena.
Rais Malinzi alisema Bwana Idd Mshangama  atakaimu nafasi hii kwa sasa mpaka mtu mwingine atakapopatikana.

Pia nafasi ya Mkurugenzi wa ufundi imebaki wazi baada ya waombaji wote kutokidhi vigezo, hivyo Bwana Salum Madadi atakaimu nafasi hiyo na Rais Malinzi ameagiza itangazwe tena na walioomba wasiombe tena.

Nafasi nyingine iliyobaki wazi ni Mkurugenzi wa fedha na utawala, hivyo itatangazwa tena na kwasasa Bwana Danny Msangi atakaimu.
Afisa habari wa TFF ataendelea kuwa Bwana Boniface Wambura Mgoyo.

Rais Malinzi alisema ajira zote zitaanza rasmi januari Mosi mwakani na anawatakia kazi njema, huku akiwa na imani kubwa kuwa watasukuma mbele gurudumu la maendeleo ya mpira wa miguu.

Katika hatua nyingine, TFF imeteua wajumbe wa kamati ya uchaguzi na kamati ya Rufani ya Uchaguzi na kamati ya soka la ufukweni.
Kamati ya uchaguzi inaundwa  na Mwenyekiti, Wakili Melchesedek Lutema, Makamu wake, Wakili Walter Chipeta na Wajumbe Hamidu Mahmoud Omar, Jeremiah John Wambura na Hassan Dalali.

Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF itakuwa chini ya Mwenyekiti , Wakili Julius Lugaziya, Makamu wake,  Wakili Mwita Mwaisaka na Wajumbe Juma Abeid Khamis, Rashid Dilunga na Masoud Issangu.

Na kamati ya Soka la Ufukweni itakuwa chini ya Mwenyekiti Ahmed Mgoyi, makamu mwenyekiti, Shafii Dauda  na Wajumbe Deo Lucas, Juma Mgunda, Boniphace Pawasa, Joseph Kanakamfumu na John Mwansasu.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA CCM DMV KUJIUZULU KWA KATIBU MKUU, JACOB KINYEMI

Emmanuel Nchimbi ,Shamsi Vuai Nahodha Bado Wanaweza kuwania urais

0
0
 

Emmanuel Nchimbi
Shamsi Vuai Nahodha
------
 Baadhi ya wasomi nchini wamesema kwamba licha ya hatua iliyochukuliwa na Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri wanne, kugusa mustakabali wa kuwania urais wa miongoni mwa wanasiasa hao katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, wanaweza kuwania nafasi hiyo kwa kuwa waliwajibika kisiasa.
           
Mawaziri walioenguliwa kutokana na athari za Operesheni Tokomeza Ujangili ni wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.
           
Wakati Nchimbi akitajwa kuwa mmoja wa wanasiasa tishio katika mbio za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao, Nahodha anatajwa kuwa mmoja wa wale watakoingia katika kinyang’anyiro cha nafasi hiyo upande wa Zanzibar lakini baada ya Dk Shein kumaliza muda wake wa vipindi viwili.
       
Katika msingi huo, gazeti hili liliarifiwa kuwa baada ya tangazo la kutenguliwa kwa uwaziri wao, baadhi ya kambi zinazojiwinda kwa ajili ya kuwania nafasi za juu za uongozi wa nchi 2015, zilishangilia na kuandaa tafrija za kupongezana.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea........

ZITTO AENDELEA KUMBOMOA DK. SLAA KWA MAKOMBORA MAZITO MAZITO ... AANIKA SIRI MPYA

0
0


Mbunge wa Kigoma kaskazini, Zitto Kabwe akihutubia Wakazi wa Kijiji cha Bitale alipokuwa katika ziara ya kutembelea baadhi ya Vijiji.Picha na Anthony Kayanda  
---
 .Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe, amejibu mashambulizi kwa viongozi wa Chadema, kutokana na kile alichosema wanazunguka na kusema maneno yasiyo ya ukweli.

Akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa Mwanga Centre, Kigoma mjini, alisema alichukua kadi ya uanachama wa Chadema mwaka 1993 wakati huo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa akiwa bado yuko CCM.
             
“Wakati hao wenye midomo mikubwa wanaoongea sasa, walipokuwa wamekumbatia watawala, nyinyi mlikuwa mnapigwa mabomu kutaka mageuzi, eti leo wao wapinzani zaidi kuliko sisi na ndiyo maana hatuwezi kuwaachia.
   
Hatuwezi kukubali, hatutoki, demokrasia ni mchakato na mwenzenu nimekuwa kwenye mchakato huu. Kadi yangu ya Chadema nimeichukulia kwenye uwanja huu, tarehe moja mwezi wa nne mwaka 1993, nikiwa na miaka 16, wakati nachukua kadi yangu, Katibu Mkuu wa chama changu alikuwa yuko CCM.
          
Akizungumza kile alichosema ni uongo unaosambazwa na viongozi wa juu wa chama hicho, Katibu Mkuu Dk Slaa na Mwenyekiti wake Mbowe waligawana maeneo Mbowe akaenda Kanda ya Ziwa na Dk Slaa Kanda ya Magharibi.Kwa Habari zaidi Bofya na Endelea......

MCHEKI RAY C ALIPOHOJIWA NDANI YA MIKASI

SALAAM MAALUM ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA CCM TAWI LA LONDON/UK

0
0

 

Kwa Niaba ya CCM Tawi la Uingereza tunapenda kuungana na Wanachama,
 
 Wapenzi na waTanzania wote kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu
 za Krismas na Ujio wa Mwaka Mpya wa 2014.

 Uingereza sherehe hizi zimetukuta katika hali ya hewa yenye
 kimbunga kingi na mvua nyingi zisizoisha, na hivyo kuathiri maandalizi kwa namna moja au nyingine kutokana na vizuizi katika baadhi ya
 miundo mbinu hasa barabara na reli.
Aidha, kama inavyojulikana Ulimwenguni Ukata wa kifedha nao umeshika
hatamu. Kuyumba kwa Uchumi wa Nchi nyingi kubwa na ndogo na kuyumba
kumepelekea mfumuko wa bei za bidhaa hasa vyakula . Tatizo ambalo
limeukumba ulimwengu mzima.

Licha ya vikwazo hivi na vingine ,hatuna budi kumaliza mwaka kwa kuangalia nyuma na kuona yale mengi yaliyofanikishwa. Kwa hali hii ,
CCM UK tunachukua nafasi hii kuipongeza kwa dhati Serikali ya awamu ya
nne ya Jamahuri ya Muungano ya Tanzania kwa utekelezaji wa ilani ya  uchaguzi ya CCM.

Mfano ulio wazi ni katika miundo mbinu ya barabara ambapo asilimia
kubwa ya Nchi sasa inaunganika kwa barabara na maeneo mengi sasa  yanafikika kirahisi kwa barabara,ambazo nyingi zimejengwa kwa kiwango cha lami. Hii imesaidia  sana kupeleka mahitaji muhimu vjijini na uvutiaji katika uwekezaji, na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

 Tunapenda kuwasihi WaTanzania wenzetu , tutumie kipindi hiki cha
 mapumziko ni vyema pia kutafakari na kupongeza yale mazuri yaliyofanywa na serikali na vilevile kuungana pamoja na kuchangia katika kuleta Maendeleo ya
 Mtanzania na si kubeza juhudi za maendeleo kwa sababu ya tofauti za
 kiitikadi na za kisiasa .

Ni muhimu kwanza tujipongeze wenyewe kama watanzania kwa nafasi pekee
tuliyonayo na tunayojivunia ya amani ya nchi yetu. Tusikubali kurubuniwa
kwa namna au hali ya aina yeyote na hasa inapobidi tujiulize na
kutafakari ni nini kinatufanya watanzania tukawa wamoja , vilevile kudumisha Amani, Umoja na Upendo wetu.

WaTanzania hatuna budi kulinda amani ya nchi yetu na upendo miongoni
mwetu kwa gharama yeyote ile na bila kuyumbishwa au kutetereka ili  tuweze kuachia vizazi vyetu vijavyo Urithi ulio mwema kuliko wowote Ule.  TANZANIA yenye Amani, Upendo na Utulivu.
"MUNGU IBARIKI TANZANIA"

BREAKING NEWSSSS ... POLISI WAUDAKA MWILI UKIWA NA KETE 17 ZA MADAWA YA KULEVYA

0
0
Maiti ikiwa ndani ya gari aina ya SPACIAL yenye namba ya usajili T 887 BSW eneo la nje ya chumba cha kuhifadhia maiti cha hospotali kuu ya mkoa wa Morogoro, baada ya gari hilo kukamatwa majira ya saa 7 usiku eneo la Mikumi,likiwa na watu watatu na maiti ya binadamu inayodaiwa kupoteza maisha baada ya kumeza kete hizo za zinazodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya na kufariki dunia, ikisafirishwa kutoka Tunduma mkoani Mbeya kwenda Jijijini Dar es Salaam. PHOTO/MTANDA BLOG.

Polisi wakiendelea kupekua gari hilo.
HIZI ndizo kete zinazodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya yaliyopatikana katika gari baada ya kupekuliwa kituo kikuu cha polisi.
MWILI wa marehemu, Khalid Abdul Kitala (47) ambaye ni mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro muda mfupi kabla ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi na kukutwa na kete 17 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya katika tukio la kufasarisha maiti iliyotiliwa shaka na askari polisi Mikumi ambao waliweka mtego kufuatia kupata taarifa za tukio hilo na raia wema na kulinasa gari lililokuwa likitokea Iringa kwenda Dar es Salaam majira ya saa 21:26: HRS jana usiku. PHOTO/MTANDA BLOG.


Katika gari la watuhumiwa lilipekuliwa kwa kina na kupatikana kete 7 na kete 17 na kufanya jumla yake kuwa 24 zilizokamatwa na watuhumiwa wapo chini ya ulinzi katika kituo kikuu cha polisi kwa uchunguzi.

Credit: Mtanda blog

BAADA YA KUTEMWA, RIDHIWANI KIKWETE AMTUMIA UJUMBE ALIYEKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI EMMANUEL NCHIMBI

0
0
Ridhiwani Kikwete (katikati) na Emmanuel Nchimbi (kulia)


Kwenye akaunti yake ya Facebook , Ridhiwani Kikwete ameandika hivi:
 
"Ni hakika kazi nzuri ,Ulipa.Ninakupa moyo kaka yangu na mpiganaji wa ukweli.

Unaposherehekea siku yako ya kuzaliwa Angalia nyuma kwa changamoto na Mbele kwa matumaini.Tuko pamoja kaka. sana na nakutakia kila la kheri"

MAZINGAOMBWE YA CHADEMA JIJINI MWANZA....VURUGU KUBWA ZAIBUKA KATI YA MEYA NA MADIWANI WA CHADEMA ... NGUMI NJE NJE

0
0


 
ILIKUWA ni kama uwanja wa vita na mipasho, ndivyo unavyoweza kusema, baada ya kuibuka vurugu kubwa kati ya Meya wa Halmashauri ya Ilemela, Henry Matata na madiwani wake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). 
Vurugu hizo ziliibuka jana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela baada ya Matata kuwataka madiwani watatu wa Chadema kutoka nje ya ukumbi kwa kuwa tayari alikwishawafukuza hivyo si madiwani tena.
  Madiwani waliotakiwa kutoka nje ya ukumbi na Kata na zao katika mabano ni Marieta Chenyenge (Ilemela), Abubakar Kapera (Nyamanoro) na Daniel Kahungu (Kirumba). 
Hali hiyo ilizua tafrani kwa pande zote mbili kwani walikuwa wakishambuliana kwa maneno makali na ya kashfa huku Meya Matata akitumia nafasi yake kuwaamrisha polisi waliokuwapo ndani ya ukumbi huo kuwatoa nje madiwani hao nguvu. 
“Nasema leo hamtakaa ndani ya ukumbi huu na lazima mnijue mimi ndio Meya wenu na posho hamtapata, naomba polisi watoeni nje na mkishindwa nitawaita mabaunsa wangu waingie ndani. 
“Wengine hapa mmekuwa mkiombana posho na ndizo zinazowaleta hapa, watu sio madiwani lakini mnang’ang’ania kuja kwenye vikao,”alisema Matata kwa ukali. 
Wakati Matata akitoa kauli hizo, madiwani hao nao walikuwa wakimjibu wakidai kuwa hata yeye si diwani wa Chadema, hana kadi na kwamba chama hakimjui na wanashangaa kuona akiendelea kuwa Meya wa Ilemela. 
Hata hivyo wakati vijembe hivyo vikiendelea, polisi walishindwa kuwatoa nje madiwani hao na baada ya kutetea haki yao ya kuwamo ndani ya kikao hicho kwa kutumia vifungu kadhaa vya sheria. 
Sekeseke lilizidi kupamba moto, pale kitabu cha kujiorodhesha majina kilipofika kwa madiwani hao kwa ajili ya kujiandikisha, jambo ambalo lilimfanya Matata amuagize muhudumu wa Manispaa hiyo kuwanyang’anya. 
Hata hivyo muhudumu huyo aliposhindwa kuwanyang’anya kitabu hicho, Matata aliomba msaada kwa polisi ambao nao walikataa hali iliyomfanya ainuke katika kiti chake na kwenda kukichukua kwa nguvu. 
Hali ndani ya ukumbi iliendelea kuwa mbaya pia baada ya madiwani hao kunyimwa majoho na taarifa za vikao huku wenzao wa CCM wakipewa huduma zote kitendo ambacho kilionekana kuwakera. 
Visa vya Matata havikuishia hapo kwani pia aliamuru meza na viti vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili ya madiwani kuhamishwa na kuvisogeza mbele karibu na meza kuu isipokuwa vile vilivyokaliwa na madiwani wa Chadema ambavyo viliachwa nyuma. 
Katika hali isiyo ya kawaida madiwani hao nao waliamua kuhama walipoachwa na kwenda pale walipokaa madiwani wenzao. 
Kitendo hicho kilionekana kumkera Matata na kuamua kutoka nje huku akisema anawafuata makomandoo wake jambo ambalo lilizua hofu kwa baadhi ya wajumbe wengine ambao walikimbilia nje. 
Wakati wote wa vurugu hizo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Zuberi Mbyana na Naibu Meya, Sule Debe walikuwa kimya mbele ya meza kuu. 
Hata hivyo muda mchache baada ya Matata kutoka nje, Mkurugenzi na Naibu meya nao walitoka nje na kutelekezwa kikao kwa zaidi ya saa moja kabla ya kurejea tena ukumbini. 
Baada ya kurudi ukumbini bila makomandoo, kikao kiliendeshwa bila kuwapa nafasi madiwani wa Chadema kuhoji wala kupewa taarifa zozote za vikao licha ya kunyoosha mikono kuhoji hali hiyo. 
Kitendo hicho kiliwafanya Madiwani wa Chadema kuwa kama wasikilizaji kwa zaidi ya nusu saa na baadaye kuamua kutoka nje na kwenda Ofisi ya Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia kufanya kikao cha dharura na kutoa tamko. 
Wakati kikao cha Chadema kikiendelea, Meya, Mkurugenzi na Naibu Meya waliendelea na kikao hicho kilichokuwa na ajenda ya kupitisha mapendekezo ya kuzigawa tarafa na kata za Wilaya ya Ilemela. 
Baada ya kumalizika kikao hicho, Matata alisema alishindwa kuingiza makomandoo wake kutokana na kushauriwa na viongozi wanzake huku akisisitiza kuwa kamwe hawezi kuwaruhusu madiwani hao kuingia kwenye vikao wakati alikwishawafukuza. 
Pia aliwalaumu polisi kuzembea kuchukua hatua pale wanapoagizwa huku akimtaka Mkurugenzi kujipanga vema na kuweka ulinzi wa kutosha wakati wa vikao vya aina hiyo. 
Tamko la Chadema 
Katika taarifa yao waliyoitoa baadaye jana baada ya kikao chao, Madiwani hao wa Chadema walidai kuwa kilichokuwa kikitokea kati yao na Meya ya Halmashauri hiyo ni mkakati wa serikali kutaka kuihujumu Halmashauri ya Ilemela ili isifikie malengo yake. 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kiongozi wa Operesheni Kanda ya Ziwa Magharibu, Tungaraza Njugu alisema vurugu zinazotokea Mwanza ni matokeo ya udhaifu wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Tamisemi na Rais Jakaya Kikwete. 
“Kinachoendelea hapa ni hujuma ambayo inaanzia kwa Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Waziri Mkuu, Tamisemi na Rais, mkakati huu wameupanga na kumweka Meya Matata kihuni wakati si diwani. 
“Leo hii ni mwaka mzima wananchi wa Ilemela hawana huduma yoyote na barabara zao mbovu, shida hii ni kwa sababu wamekosa wawakilishi badala yake kumeundwa genge ndio linaloendesha Halmashauri. 
“Chadema Mkoa  wa Mwanza tunaungana kuhakikisha Pinda anaondolewa madarakani kwa sababu ya kushindwa kuziongoza hizi Halmashauri na badala yake analea uchafu” alisema. 
Kwa upande wao, madiwani hao walisema wao ni madiwani halali na hata Pinda alitangaza kupitia Bunge lililopita kwamba anawatambua huku wakidai kuwa barua za wao kutambulika zipo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. 
Rai jumatano

FILIKUNJOMBE , KANISA WATUMA SALAM ZA KRISMAS KWA JK

0
0

KANISA  la Anglicana   Ilela kata  ya  Ilela wilaya ya  Ludewa  mkoani  Njombe  limetuma  salam  za krismas  na mwaka mpya  kwa  Rais  Jakaya  Kikwete  kwa  kumpongeza kwa  kumaliza mgogoro  wa mpaka  kati ya Malawi  na Tanzania  katika eneo la Ziwa Nyasa kuwa  kwa  sasa  wanaishi  bila  hofu  yoyote.
Huku  mbunge  Deo  Filikunjombe  akimpongeza  Rais Kikwete  kwa  kutimiza ahadi  yake ya gari  la  wagonjwa  katika Hospital  ya wilaya ya  Ludewa ahadi  ambayo  aliitoa  wakati wa ziara  yake.
 
Mbali  ya salama  hizo  pia  kanisa  hilo  limempongeza Rais  Kikwete  kwa utendaji  kazi mzuri  pamoja na  kutengua uteuzi  wa  mawaziri  wanne  ambao ambao  wizara  zao  zilitajwa kushindwa  kufanya  vema katika oparesheni  tokomeza.
Akitoa  salam  hizo jana  wakati  wa  ibada  ya  krismas ambayo  ilihudhuliwa  pia  na  viongozi mbali mbali wa chama  na serikali  wilaya ya  Ludewa  pamoja na  mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe mchungaji wa  kanisa  hilo  Camon Ngoye  alisema wanatambua  mchango wa  serikali  ya rais  Kikwete.
Alisema  kuwa  awali  wakati  wa  choko  choko ya  mgogoro  wa mpaka   kati  ya  Tanzania na Malawi  wananchi wanaoishi  jirani na mwambao wa  ziwa Nyasa  walikuwa  wakiishi  kwa hofu  kubwa.
“Sisi  kama kanisa  tunatambua  kazi  kubwa  iliyofanywa na Rais  Kikwete  katika  kulitumikia  Taifa  na pili  tunashukuru sasa  hivi  hakuna hofu  ya mpaka wa  ziwa  nyasa tena”
Pia  alisema  kuwa  jambo  jingine  ambalo  linalifanya kanisa  hilo  kumpongeza  Rais  ni kuwawajibisha  viongozi hasa  mawaziri ambao uwajibikaji  wao  ulionekana  

Kwa  upande  wake  mbunge  Filikunjombe  alimpongeza  Rais  Kikwete  kwa  kutekeleza ahadi  yake ya  gari la wagonjwa katika  Hospital ya  wilaya ya Ludewa ahadi ambayo ameitimiza.

Alisema  kuwa gari  hilo ni msaada  mkubwa  kwa  wilaya ya  Ludewa na  kuwa moja kati ya  salam za JK kwa  wana Ludewa ni pamoja na gari  hilo.

Hata  hivyo alisema Rais Kikweete anataraji  kufika katika  eneo la Manda mapema mwakani  .

Akielezea  kuhusu uamuzi  wake  wa kuendelea  kuzunguka katika maeneo  mbali mbali  ya  jimbo  hilo alisema ni kuhamasisha  jamii  kujenga upendo  na faraja  kwa  wagonjwa.
Credit: matukio blog

MBONI AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA MKOANI IRINGA KUSHEREKEA SIKUKU YA CHRISTMAS

0
0





Mtangazaji  maarufu  wa kipindi cha Mboni Show kinachorushwa na  kituo  EATV  Bi Mboni A .Masimba anataraji  kula  sikukuu ya Krismas na mwaka  mpya  na  watoto   yatima mkoani Iringa .
 Akizungumza  ,Mboni amesema  kuwa akiwa kama mtanzania na mwanahabari ameamua  kuandaa chakula  cha  pamoja  na  watoto  yatima  wa  vituo  vitatu vya mkoa wa  Iringa .
 
Alisema  kuwa  hafla  hiyo  ya  kula  chakula na yatima  itafanyika  siku  ya Desemba 25 mwaka  huu ambayo  itakuwa ni sikukuu ya Krismas .
Bi Mboni  alisema  kuwa  mbali ya  kuendesha  vipindi  vyake  katika kipindi  chake cha  Mboni Show bado ameguswa  kula pamoja na  watoto  hao 230  pamoja na wageni  mbali mbali  watakaofikisha idadi  ya watu 300.
Alisema  kuwa  hafla  hiyo  itafanyika katika ukumbi wa Hihglands mjini  Iringa  na  kuwa  vituo ambavyo vimealikwa ni pamoja na TOSAMAGANGA , Upendo Centre  Sabasaba na YATIMA MOYO KWA MOYO  kilichopo Mufindi kata ya  Bumilayinga

Hata  hivyo  alisema mbali ya  chakula  hicho   pia  watoto  hao  yatima  watapata  zawadi mbali mbali  kutoka kwake.
Mboni  amesema  kuwa  amekuwa  bega kwa bega na watoto  yatima  na  kuwa mbali  ya kula na  watoto  hao pia  amekuwa akifanya  hivyo wakati  wa sherehe  za Ramadhan pia  kutokana na kipindi  chake  kutazamwa na  watanzania  wote .
Hivyo  alisema  lengo  kuu ni kuwakumbusha  watanzania  juu ya  kuwakumbuka  watoto  yatima  kama  ambavyo  wamekuwa  wakichangia sherehe mbali mbali .
 
 
Na mtandao  wa www.francisgodwin.blogspot.com
 

MWANAMKE AOZA MAKALIO YALIYOSABABISHWA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KUONGEZA MAKALIO

0
0

 


Adha hii imempata mwanamke huyu baada ya kuanza kuona ngozi yake imeanza kuwa laini kasi kwamba alianza kumomonyoka taratibu mwisho wa siku alijikuta ameoza wanawake wengi huwa wanajikuta wanaingia katika taabu hizi kwa kufuata mkumbo

MWANAFUNZI MWINGINE CBE AFARIKI DUNIA

0
0

MAREHEMU SAMWEL P. KITULA
Ikiwa ni siku moja imepita Tangu Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dodoma kiondokewe na aliye wahi kuwa Mwanafunzi wa Chuo hicho katika Level ya Diploma 2012/2013 Marehemu Zeinabu J. Kasenga (ODMK -2012/2013)

Simanzi zimezidi kutanda Chuoni hapa baada ya Mwanafunzi Mwingine Bw. Samwel P. Kitula (37) aliyekuwa akisoma Bachelor Degree in Procurement and Supplies Management mwaka wa tatu (3) mkondo "A" Kufariki Dunia usiku wa kuamkia Tarehe 26/12/2013 ( Mnamo saa 8 usiku) katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital).

Kwa mujibu wa Msemaji wa Familia amesema Marehemu alikuwa akisumbuliwa na Matatizo ya Ini mpaka kupelekea Mauti yake.

Kwa upande wake Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Dodoma Mhe. Remidius M. Emmanuel amesema Amepokea taarifa hiyo kwa majonzi makubwa sana na kuwataka wanafunzi wote kuwa wavumilivu hasa katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mwanafunzi mwenzetu. Hata hivyo Rais huyo amewataka wanafunzi kuwa watulivu wakati taratibu mbalimbali zinaendelea na kila kitakachoendelea watafahamishwa kupitia taratibu mbalimbali za mawasiliano hapa chuoni.Ingawa amasema Marehemu amekuwa akiishi na familia yake eneo la Makole karibu kabisa na Lodge ya ELGON, hivyo ni vema kila mtu kwa nafasi yake kujongea eneo hilo kwa ajili ya kutoa pole kwa Familia ya Marehemu.

MKE ADAIWA KUMUUA MUMEWE

0
0

Na Mwandishi Wetu
SHETANI anazidi kuuatamia ulimwengu! Mama mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Farida mkazi wa Mburahati jijini Dar, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudaiwa kumuua mumewe aliyetajwa kwa jina la Amosi Joseph kwa kumpiga kwa kukombe kichwani, Ijumaa linaidondosha kama ilivyo.
Akisimulia mbele ya gazeti hili mkasa mzima, mtoa habari hii aliyetajwa kuwa dada wa marehemu anayejulikana kwa jina la Khadija, alisema siku ya tukio kaka yake aliamka asubuhi na kumuaga kuwa anakwenda bondeni kwa mkewe (Farida) kwa kuwa walikuwa nyumba tofauti.
Aliongeza kuwa, muda mfupi baada ya kaka yake kuondoka nyumbani hapo, wifi yake (Farida) alifika nyumbani hapo na kumwambia kuwa kaka yake ameumia sana aende akamuone.

“Mimi nilimshauri ampeleke hospitali tu nikidhani ameumia kidogo, kwa sababu wamekuwa na kawaida ya kupigana mara kwa mara na tulishawaonya. Wifi aliondoka na mimi nikaendelea na shughuli zangu.
“Muda mfupi, uliingia ujumbe kwenye simu yangu ya mkononi ukisomeka kuwa kaka yangu alikuwa amefariki dunia huku ujumbe huo ukinionya kutolia ili nisimshitue mama,” alisema Khadija.
Dada mwingine wa marehemu aliyejulikana kwa jila la Christina, alisema yeye aliwahi kufika nyumbani kwa Farida na kumkuta kaka yake akiwa amelala chali huku damu zikimvuja, muda mfupi polisi waliwasili na kufanya taratibu zote muhimu.
Marehemu Amoni alizikwa siku chache baada ya kufariki dunia kwenye makaburi ya Mburahati City jijini Dar huku Farida akiwa mikononi mwa polisi kwa upelelezi zaidi.
Gazeti hili linaipa pole familia ya marehemu na linamuomba Mwenyezi Mungu ailaze pema roho ya marehemu Amosi-Amin.

                GPL

Lipumba: Hali ya uchumi ni mbaya, Serikali ichukue hatua

0
0

 


uchumi
Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza na waandishi wa Habri jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa tamko la kulaani kwa kitendo cha Naibu Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwazalilisha Wabunge wa upinzani akiwepo Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Picha na Venance Nestory 
…………………………………………………………………………………
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka Serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka wa matatizo ya kiuchumi, kwa kuwa hali ilivyo sasa ni mbaya.
Profesa Lipumba ambaye pia ni profesa wa uchumi alisema hivi karibuni Dar es Salaam kuwa hali ya uchumi imezidi kudorora na kusababisha maisha ya wananchi wengi kuwa magumu.
“Vijana wa siku hizi wengi hawana simile kushughulika na mambo yanapokwenda sivyo, ajabu ni kwamba wanaofanya mambo hayo yawe magumu wamekuwa wepesi wa kutetea kwa hoja zisizo na msingi kwa masilahi yao binafsi,” alisema.

Akizungumzia maazimio yaliyofikiwa kwenye Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kilichofanyika Desemba 21-22 mwaka huu Dar es Salaam, alisema hatua ya kupandishwa kwa gharama za umeme iliyotangazwa hivi karibuni na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni miongoni mwa mambo ambayo yanaendelea kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi, jambo ambalo lingeweza kuzuilika kwa shirika hilo kudhibiti wizi wa nishati hiyo.
Kuhusu hali ya kisiasa nchini, Profesa Lipumba alisema Baraza Kuu limetoa wito kwa vyombo vya Dola kuwa na weledi na uadilifu na kuacha kutekeleza amri za wanasiasa zisizojali utawala wa sheria na haki za binadamu ili vipunguze uhasama baina yao na raia.
“Serikali pia isitumie Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kushughulikia masuala ya uvunjifu wa sheria katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, badala yake kazi hiyo ifanywe na Jeshi la Polisi kwa mujibu wa taratibu za kisheria. Nao pia waongezewe uwezo wa kiutendaji,” alisema.
Alisema CUF inaona si vyema kutumia JWTZ kudhibiti vurugu kwa kuwa wanajeshi hao hawana mafunzo ya kukamata wananchi wenye tuhuma za uhalifu isipokuwa wamefundishwa jinsi ya kulinda usalama wa nchi katika mipaka.
CHANZO: MWANANCHI
Viewing all 16721 articles
Browse latest View live


Latest Images