Quantcast
Channel: EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Viewing all 16721 articles
Browse latest View live

Wema Sepetu:Wanaoniponda Wengi Wao Wanatumia Tecno na Huawei

$
0
0
Katika hali iliyoshangaza wengi,beautiful oninye mwenye endless fame mnyange Wema Sepetu amesema watu wengi wanaomsema kwenye mtandao they don't have life na wengi wao wanatumia Tecno na Huawei kulog in kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kumponda, akichezesha taya na Ephraim Kibonde katika kipindi cha jahazi amesema watu hao hawampi shida hata kidogo kwani wamepigika na yupo juu zaidi yao.

My Take:Hivi Sister wema hizo simu ulizozidharau unazijua vizuri kweli? Hivi unaweza ku-compare features za Huawei Ascend P7/Tecno H7 na Samsung Gallaxy S4?

YAONE MAHABA NIUE YA AUNTY EZEKIEL NA CASSIM MGANGA WAKIWA KWA OBAMA

RAY AFUNGUKA KUHUSU CHUCHU NA KUTOKUJUA KIINGEREZA!

$
0
0
SI LAZIMA NIJUE KIINGEREZA 
Mkurugenzi wa Kampuni ya filamu Rj Company,Vicenti Kigosi amesema si lazima kujua Kingereza maana hata Messi hajui, Ray amesema hayo alipokuwa akichat Live na mashabiki zake kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachokukutanisha na watu mahiri kila siku ya jumatano kuanzia saa sita za mchana mpaka nane kamili. Mkali huyo ambae kwa sasa anachukuliwa kama moja ya watu wenye mafanikio katika tasnia ya filamu nchini ambae pia ameshawishi vijana kibao kuingia katika tasnia hiyo amefunguka na kuweka wazi kuwa suala la lugha ya kiingereza kwake ni changamoto lakini si jambo la ajabu sabgabu kuna watu wengi maarufu duniani wanapigwa chenga na lugha ya kiingereza. 
Prince Dully >>>>Mbona haujui kingereza au uliishia darasa la saba,nini? 
RAY Kigosi >>>>>>Hata messi hajui kiingereza kwani mimi muingereza nijue Kiingereza.
CHUCHU MCHUMBA WANGU 
Msanii Vicent Kigosi ambae katika hizi siku za karibuni ilisikika kuwa yupo katika mahusiano na msanii mwingine wa filamu ambae anafahamika kama Chuchu Hans hivyo ilipelekea mashabiki wa ukurasa wa facebook wa EATV kutaka kujua ukweli juu ya mahusiano hayo na kama kweli jamaa ana mpango wa kumuoa binti huyo au laah, na majibu ya Ray aliwataka kwamba wawe watulivu muda utakapofika ndio watajua ukweli wote juu ya suala hilo.

BUNGE MAALUM LA KATIBA LAPENDEKEZA IBARA 274 BADALA YA 271 ZA TUME .

$
0
0

j 
BUNGE MAALUM LA KATIBA LAPENDEKEZA IBARA 274 BADALA YA 271 ZA TUME .
  • IBARA 186 ZA TUME ZABORESHWA
  • IBARA 41 MPYA
  • IBARA 47 ZA TUME ZABAKI KAMA ZILIVYO
  • IBARA 28 ZA TUME ZAFUTWA
Na Mwandishi wa MAELEZO-Dodoma
Bunge Maalum la Katiba limependekeza jumla ya Ibara 274 katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayopendekezwa.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum Mhe. Andrew John Chenge wakati akiwasilisha Bungeni Rasimu ya Katiba inayopendekezwa katika Kikao cha Arobaini na mbili.
Amesema kuwa wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba inawasilisha Bungeni Rasimu Katiba inayopendekezwa iliwasilisha Ibara 271.

Mhe. Chenge amesema kuwa baada ya kupitia Rasimu Katiba ya Tume walifanikiwa kupata Ibara 274 ambazo ndio wanapendekeza ziwemo katika Katiba mpya ijayo.
Ameongeza kuwa kati ya hizo zilizopendekeza na Bunge Maalum la Katiba 233 zimetokana na mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyowasilisha Bungeni mwezi Machi mwaka huu.
Amesema kuwa katika Ibara 47 kati ya zote za Tume 47 hazikufanyiwa marekebisho badala yake zilibaki kama zilivyopendeza wakati Ibara 186 ndio zilifanyiwa maboresha na marekebisho kwa ajili ya kuziboresha na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
Mhe. Chenge ameongeza Bunge hilo limeongeza Ibara 41 mpya na kufuta 28 zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
 Rasimu ya Katiba inayopendekeza na Bunge Maalum la Katiba ina sura mpya mbili mpya ambayo ni ardhi ,maliasili na mazingira na sura inayohusu Serikali ya Mapinduzi ya Mapinduzi, Baraza la Mapinduzi na Baraza la Mawakilishi.

TRANSFOMA ZA TANESCO ZILIZOUNGUA BAADA YA KUIBWA MAFUTA NA KUSABABISHA HASARA YA BILIONI 1.4

$
0
0


 Afisa usalama wa shirika la umeme nchini Tanesco Cyprian Lugazia akiwaonyesha waandishi wa habari transifoma zilizoungua baada mafuta yake kuibwa na kulisababishia hasara shirika hilo Ya jumla ya shilingi bilioni 1.4 katika kipindi cha miezi minne tangu April mwaka huu.(Picha na Kenneth Ngelesi)
 Transfoma ziliungua baada ya mafuta yake kuibwa na vishoka na kulisababishia shirika hilo hasara jumla ya shilingi bilioni 1.4 katika kipindi cha miezi minne kuanzia April mwaka huu.
Transifoma mali ya shirika la umeme nchini (TANESCO) yakiwa yameungua baada ya kuibwa mafuta na kulisababishia hasara shirika hilo zaidi ya shilingi bilioni 1.4 katika kipindi cha miezi minne tangu April mwaka huu

Isome Rasimu iliyopendekezwa na Kuwasilishwa katika Bunge Maalum la Katiba na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA Diploma and Certificate CHUO KIKUU MZUMBE YAMETOKA

Madee atoka nje kwa dhamana baada ya kuhusishwa na tukio la utekaji

$
0
0

Muimbaji wa Tip Top Connection, Madee hivi karibuni alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuwekwa ndani katika kituo cha polisi cha Kigamboni kutokana na madai ya kuhusishwa na tukio la utekaji.
 
Kabla ya kuongea na meneja wa kundi hilo, Babu Tale, mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown aliripoti kupitia ‘You Heard’ ya XXL kuwa Jumamosi iliyopita Madee aliporwa simu yake na watu wawili usiku huko Kigamboni
 
Babu Tale alisema: "Kwenye mida ya saa tisa usiku Madee wakati anatoka kwenye show Kigamboni kuna waporaji simu wakiwa kwenye pikipiki wakampora,kwahiyo ikabidi gari aliyokuwemo Madee ikiendeshwa na Kwebe ianze kuikimbiza ile pikipiki halafu wakaigonga pikipiki kwa nyuma.
 
"Pikipiki ilivyodondoka yule aliyekua nyuma kwenye pikipiki ambaye ndio alipora simu akafanikiwa kukimbia hivyo wakaishia tu kumkamata aliyekuwa anaendesha hiyo pikipiki.
 
“Wakamchukua na kwenda nae maskani TipTop,” ameeleza Tale. 
 
Mama yake akaja akasema,"msipeleke polisi mwekeni hapa mi nakwenda kuwachukulia vitu vyenu. Madee kwa sababu alikua anakwenda kwenye show Mwanza ikabidi aende zake, saa nne asubuhi yule mama akaja na polisi badala ya kuja na mwizi, mwenzake akaja na polisi kataka kuwaokota watoto wote ofisini kwangu pale Tiptop.
 
" Walimchukua huyo mhalifu kwenye Land Rover mpaka Polisi Magomeni na kubadilisha kibao kwamba huyu mtuhumiwa alitekwa.”
 
“Alipigwa akaumia hivyo wakamuombea PF3 wakampeleka hospitali. Nikapigiwa simu na Madee kwamba anatakiwa polisi akaripoti, kufika kituoni wakakuta ile pikipiki na kukuta yule dogo ndio anafika kutoka hospitali akawaambia ‘huyu ni mwizi ameiba’ Ikabidi dogo aingizwe ndani jana akalala pale polisi Magomeni.
 
“Asubuhi yake Madee akaenda kituoni kama kufuata mhalifu wake na kutaka simu yake aliyoibiwa, akaambiwa kesi inabidi ihamishiwe Kigamboni. Saa kumi na mbili jioni ndio Kwebe ananitumia meseji anasema Madee analalamika mbona humfatilii, nikauliza ‘kuna nini tena’ akasema wamemuingiza ndani. 
 
"Nikapiga simu polisi Kigamboni ndio wakaniambia kijana wako tulitaka kumtoa lakini hatuwezi sababu amemteka mtu. Nikapiga simu kwenye vyanzo vyangu vya msaada tukamtolea dhamana, ni hilo, yataisha kama yalivyoanza"-Babu Tale
 
Source:Millardayo

Wafuasi watano wa CHADEMA Mbaroni

$
0
0

Wafuasi watano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usio halali.

Wafuasi hao akiwemo Mratibu wa Chadema Kanda ya Magharibi, Christopher Nyawanji wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Verynice Kawiche.
 
Washtakiwa wengine ni Laurent Manguweshi ambaye ni katibu wa Chadema Mkoa wa Katavi, Agnes Stephano mkazi wa Dar es Salaam, Elisha Daudi Mkazi wa Tabora na Tuli Kiwanga ambaye ni Katibu wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) Mkoa wa Dodoma.
 
Akisoma mashitaka hayo, wakili wa Serikali, Chivanenda Luongo alidai watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Septemba 18 mwaka huu katika Manispaa ya Dodoma.
 
“Watuhumiwa wanashitakiwa kwa mashitaka mawili la kufanya mkusanyiko usiokuwa halali na kukaidi amri halali ya Kamanda wa Polisi wa Wilaya (OCD) ya kutowataka waandamane,” alisema.
 
Washitakiwa hao ambao wanatetewa na mwanasheria Tundu Lissu wamekana mashitaka yao na wako nje kwa dhamana hadi kesi yao itakapotajwa tena Oktoba 22 mwaka huu.
 
Akizungumza nje ya mahakama, Lissu amesema watuhumiwa hao walikuwa wanatoka Dar es Salaam kwenye mkutano mkuu wa chama wakielekea kwao.

Hivi ndivyo Mwigulu anavyo SHARE love na Wananchi wake huko Iramba

$
0
0


Comrade Mwigulu Nchemba akiwa amembeba Mtoto katika kijiji cha kaselya wakati alipotembelea kukagua Usambazaji wa Nguzo za Umeme na Waya Jimboni Iramba.
 Mh,Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mama huyu Mlemavu wa Ngozi ambaye Mwigulu amekuwa akimsaidia katika Maisha yake,Hapa Mama huyu amebarikiwa kupata mtoto hivyo anamuonesha Mbunge wake hapa Iramba,Comrade Mwigulu Nchemba akimsikiliza Mwananchi wake mwenye Ulemavu katika kijiji cha Ndulungu Jimboni Iramba.Mh.Mwigulu Nchemba akipokea zawadi ya Kibao kilichonakishiwa kwa maneno "MH:MWIGULU MKOMBOZI WA IRAMBA|".Hakika kwa sasa Jimbo la Iramba limefanikiwa kupata miradi ya maendeleo mingi ikiwamo Umeme,Barabara,Hospitali na shule kwa kiwango kikubwa hazijawahi kuwepo Iramba,Hivyo juhudi za Mbunge zimepelekea Iramba sasa kusambazwa Umeme Vijiji vyote.

Mmoja ya Wanafunzi ambao Mwigulu amepata kuzungumza naye kuhusu masomo na hali ya shule,Mwigulu anasomesha watoto waliokatika mazingira magumu zaidi ya 300 jimboni kwake,Wengine wameshahitimu kidato cha sita.
Vijana wakiteta na Mbunge wao kuhusu Vifaa vya Michezo.Comrade Mwigulu Nchemba akisikiliza kwa makini tatizo la huyu mama na mtoto wake katika kijiji cha Ndulungu Jimboni Iramba.

Hii ni sehemu tu ya Furaha ya Wananchi wanapokutana na Mbunge wao ambaye amewaletea maendeleo hapa Iramba ambayo yalikuwa ni ndoto kwao,Ujenzi wa shule,Maabara,Umeme,Zahanati kila kata,Barabara nk
Picha/Maelezo na Sanga Jr.

SERIKALI YAWATEMA WAANDISHI WALIOPIGWA,YASEMA HAKUNA MWANDISHI ALIYEPIGWA WOTE NI WANACHAMA WA CHADEMA

$
0
0



Na Karoli Vinsent
  HUKU wadau mbalimbali wa Habari wakiwa wanalaani Vikali kitendo cha Jeshi la polisi kuwapiga wanahabari wakati wakiwa kazini,tukio hilo lilitokea Mwishoni mwa wiki iliyopita Makao makuu ya Jeshi la polisi nchini ambapo mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe alipofikishwa  polisi,
        
           Katika hali ya kushangaza Serikali imesema haina taarifa juu ya kupigwa kwa mwandishi,bali imesema inafahamu tu wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ndio waliokwenda makao makuu ya Jeshi la Polisi,na hawafamu kwamba kunawanahabari waliopigwa,

            
         Kauli hiyo ya Kushangaza imetolewa leo jijini Dar Es  Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo,Asah Mwambene wakati alipokuwa anatembelea Mradi wa Maendeleo wa Shirika la tanesco uliopo Mbagala Jijini Dar Es Salaam,licha ya kuzungumia masuala mbalimbali kuhusu Tanesco kufikisha Miaka 50 ya kutuo huduma,
          
          Ndipo Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi alipomuuliza Mkurugenzi huyo kwamba yeye kiongozi wa Waandishi wa habari anazungumziaje kitendo cha Jeshi la Polisi kuwapiga waandishi wa habari walipokuwa kazini wiki iliyopita.
         
         Ambapo Mwambeni ambaye  vilevile pia ni Msemaji wa Serikali alisema hana taarifa za kupigwa waandishi wa habari bali anacho fahamu yeye ni wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema walikwenda polisi.
    
           “Serikali haina taarifa za kupigwa kwa waandishi Serikali inachojua ni wanachama wa chama cha Chadema ndio walikwenda kwenye jeshi la polisi na sio waandishi wa habari,na tunachojua sio waandishi wa habari waliopigwa,nakuomba tuzungumeze vitu vingine ”Alijibu Mwambene.
         
              Baada ya Mwambene kuzungumza kauli hiyo,alitoka pembeni akawa anaongea na Mwandishi wa Gazeti la Habari leo ambaye naye ni Miongoni mwa Waandishi wa Habari waliopigwa na jeshi la polisi katika Tukio hilo huku akirekodiwa na mwandishi wa Mtando huu bila ya yeye kujua kwamba mwandishi wa Mtandao huu anayafuatilia mazungumo hayo alisikika akisema

        “Ni mwandishi mmoja tu anayelalimika  sana kwenye Vyombo vya Habari,ni Yule Josephat isango wa gazeti la Tanzania daima Yule tunajua kabisa ni mwanachama wa chadema kabisa maana aliwai kugombania Ubunge kupitia chama hicho na tunachojua sisi na hata polisi waliokuwa wakimpiga wanamjua Yule ni chadema ndio maana wakampiga unategemea serikali tufanyaje “alihoji Mwambene.
          
           Kauli hiyo ya Mwambene inatafsiriwa tofauti na wadau wa Masuala ya Habari kwani kuzungumza huku kunazidisha maswali mengi kutokana na Idara ya habari maelezo ndio inayowasimamia Waandishi pamoja na Magazeti.
   
             Kwa Upande wake Mwandishi ambaye anashutumiwa na Mwambene Josephati Isango wa Gazeti la Tanzania Daima,wakati alipokuwa anafanyiwa mahojianao maalum na Mwandishi wa Mtandao huu jana jijini dare s Salaam,ambapo alisema kwa sasa anajipanga kwenda mahakamani kumburuza mahakamani Cp Chagonja,Polisi watatu waliompiga pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

          “Nasahivi nawasiliana na Wanasheria wangu watatu jinsi ya kwenda mahakamani kuwashitaki polisi watatu,Cp Chagonja,waziri mkuu mizengo Pinda ambaye ametoa kauli ya pigwa tu Bungeni nafanya hivi kupata haki ya kwetu sisi waandishi Habari”alisema Isango

MAJANGA ... MAJANGA TENA ... MWENYEKITI WA CHADEMA MBEYA VIJIJINI AHAMIA ACT

DR. DRE AFUNIKA KWA PESA WANAHIP HOP FORBES

$
0
0


Daktari wa midundo, Dr Dre ameongoza orodha ya Forbes ‘Hip Hop Cash Kings 2014’ akivaa taji hilo baada ya kuingiza kiasi cha $620 million mwaka huu. 
Sio tu kwamba Dr Dre ameongoza orodha hiyo bali ameweka rekodi ya aina yake kwa kuwa kiwango alichoingiza kinazidi jumla ya fedha zote walizoingiza wasanii wengine 24 walioingia kwenye orodha hiyo mwaka huu. 
Dre anarudi kwenye nafasi yake hiyo aliyokuwa akiishikilia mwaka 2012 kabla ya kufunikwa na P. Diddy mwaka jana.

Anaongoza orodha hiyo kwa kishindo baada ya kampuni ya Apple kutangaza kuinunua kampuni anayoimiliki kwa kushirikiana na Jimmy Lovine ya Beats Electronics kwa $3 billion. 
Nafasi ya pili imeshikiliwa na Jay Z na P.Diddy ambao wamefungana kwa kuingiza kiasi cha $60 million kila mmoja. 
Jay Z ameingiza kiasi hicho kupitia matamasha mengi aliyoyafanya, biashara zake na album yake ya Magna Carter Holy Grail iliyofikia mauzo ya Platinum hata kabla haijaachiwa baada ya kampuni ya Sumsang kununua nakala milioni moja. 
P. Diddy yeye aliingiza kiasi hicho ($60 million) kupitia biashara zake mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wake wa mavazi wa Sean Jean, Revolt TV na mengine. 
Rapper wa Young Money, Drake anashikilia nafasi ya 4 katika orodha hiyo akiwa ameingiza kiasi cha $33 million. Kiasi hiki kimetokana na mauzo ya album yake ya ‘Nothing Was The Same’ iliyouza nakala zaidi ya Milioni 4 duniani kote. Kiasi kingine kiliigia kupitia endorsement ya Jordan na tour yake. 
Nafasi ya 5 imeshikiliwa na wasanii wanaofanya kazi pamoja Macklemore & Ryan Lewis ambao wameingiza kiasi cha $ 32 million. Wasanii hao walifanikiwa mwaka jana kushinda tuzo nne za Grammy kati ya saba walizokuwa wakiwania. Ushindi huo uliwasaidia kupata shows nyingi zaidi na kufanya biashara kubwa mtaani. 
Kanye West amekamata nafasi ya 6 akiwa ameingiza kiasi cha $30 million. Tour yake ya ‘Yeezus’ ilifanikiwa zaidi na kumuingizia kipato kikubwa na kumsaidia kuongeza pato la mwaka kwa asilimia 50. 

orodha kamili: 

1. Dr Dre- $ 620 Million 

2. Jay Z- $60 Million (tie) 

3. Diddy- 60 Million (tie) 

4. Drake – 33 Million 

5. Macklemore & Ryan Lewis 32 Million 

6. Kanye West- 30Million 

7. Birdman – 24Million 

8. Lil Wayne- 23Million 

9. Pharell William -22Million 

10. Eminem- 18Million 

11. Nicki Minaj- 14Million 

12. Wiz Khalifa- 13Million (tie) 

13. Pitbull- 13Million (tie) 

14. Snoop Dogg- 10Million 

15. Kendrick Lamar- 9Million 

16. Luda Cris – 8Million (tie) 

17. Tech N9ne- 8Million (tie) 

18. Swizz Beatz -8Million (tie) 

19. 50 Cent- 8Million (tie) 

20. Rick Ross- 7Million (tie) 

21. J. Cole –7Million (tie) 

22. DJ Khaled- 7Million (tie) 

23. Lil Jon- 7Million (tie) 

24. Mac Miller -7Million

Magazeti ya Leo Alhamisi Septemba 25

MTANZANIA MWINGINE ASHIKWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO NIGERIA.

$
0
0



According to report reaching us, a woman was nabbed with kilos of hard drugs. Money is very good, but the love of money is the root of all evil. Madam Chinelo just found out. The plan by the food vendor who inserted 685 grammes of cocaine in her private part, to beat operatives of the NDLEA at the Murtala Muhammed International Airport, Ikeja, has been foiled, as she was arrested. Chinelo Okorom Lynnette, 36, was arrested during inward screening of passengers on an Ethiopian Airline from Addis Ababa, Ethiopia to Nigeria.

NDLEA Head of Public Affairs, Mitchell Ofoyeju, said: ”The suspect tested positive for drug ingestion and vaginal insertion. She, however, expelled a total of 685 grammes of substance that tested positive for cocaine while under observation at the airport. Confessing after she has discharged the drugs, Madam Chinelo said "I was deceived": She told NDLEA officials at the Airport Command headed by Mr Hamza Umar that she was deceived into the illicit business out of frustration by her landlord, following her in ability to pay her rent. According to the woman, “My husband abandoned me with four children two years ago. Since then, I have been working hard to pay their school fees and also ensure their proper upkeep. I sell food at Ajagbandi to take care of my children. Photo below;

“When my rent expired, I had no money to renew it. My landlord ejected us and I had nowhere to go with the children or who to talk to. I was crying like a baby when a man came to console me. “He told me to wipe my tears and promised to introduce me to importation business. I felt he was God-sent when he sponsored my trip to Addis Ababa. Before leaving, he said I was to go into importation of female hand bags. “But when I got to Ethiopia, he told me to take cocaine to Nigeria. Initially, I disagreed but he threatened to recover his investment at all cost. I am just a victim of man’s cruelty to man.”

KINANA ATUA KILINDI, ASHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII

$
0
0


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Kwediboma wakati wa mapokezi .

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwaslimia wakazi wa Kwediboma wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kwediboma wakati wa kushiriki kujenga msingi wa kituo cha afya cha Kwediboma.

Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kutandaza mawe kwenye msingi wa kituo cha afya Kwediboma.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kumwaga zege kwenye msingi wa chumba cha mahabara ya Shule ya Sekondari Kibirashi wilayani Kilindi.
Wakina mama wa kimasai wakiwa kwenye mkutano wa hadhara Kibirashi.
 Bendera za CCM zikipepea
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kibirashi wilaya ya Kilindi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara Kibirashi,Kilindi.



Wakazi wa Kibirashi wakifuatilia yaliyojiri kwenye mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na wanachama wapya wa CCM wakila kiapo cha utiifu cha kujiunga na Chama Cha Mapinduzi.

 Hivi ndivyo Kinana alivyopokelewa Kilindi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wazee wa Songe wilaya ya Kilindi wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa mkutano.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Songe wilayani Kilindi wakati wa mkutano wa hadhara.
 Umati wa watu wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Songe wilaya ya Kilindi.
 Wananchi wa Songe wakinunua nguo za CCM,Ssre za Chama Cha Mapinduzi zinazidi kupendwa siku hadi siku .
 Hili ndio Soko la Mahindi Songe.
 Wananchi wa Songe wakishangilia jambo wakati wa mkutano wa hadhara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Songe  kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali haiwezi kufanya kila kitu hivyo hakuna ya kuongeza bidii katika kujitegemea.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinunua karanga baada ya kumaliza mkutano wake kata ya Songe wilaya ya Kilindi mkoa wa Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Songe.

Loveness Mamuya na Mrejesho wa Kwanini Usiku wa Jakaya ni Kitu cha Kujivunia Daima

$
0
0


1.   UTANGULIZI

Binadamu hakuumbwa katika ombwe, ameumbwa akiwa katika dimbwi la majukumu, kwake binafsi, familia, jamii na dunia kwa ujumla. Wachache sana wanaoweza kupitia ngazi zote za uwajibikaji huu. Katika hao wachache, hatutasita kumtaja Jakaya Khalifan Mrisho Kikwete. Ili kujijenga vema katika misingi ya uongozi, Jakaya Kikwete alijijenga vema katika taasisi hizi za msingi na alipikwa vema.

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni aina ya kiongozi pekee ambaye alihudumu nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali. Safari yake ya uongozi ilianzia ndani ya chama cha TANU. Alikuwa kiongozi wa Vijana wakati wa TANU na baadaye CCM hadi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.  Wakati wote katika nafasi zake kwenye chama na serikali, Mh. Kikwete alihimiza maendeleo katika Jimbo lake na watanzania kwa ujumla.

Kimsingi amekuwa chachu ya maendeleo katika kipindi cha urais wake kuanzia mwaka 2005 hadi 2014 ambapo ameshatekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambapo mingi imeshakamilika na mingine inategemewa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2015.

2.   HISTORIA YA MAENDELEO

Kimaendeleo, Tanzania ya mwaka 1961 si ya sasa. Tulipopata uhuru mwaka 1961, Tanzania ilikuwa ni nchi changa ambayo haikuwa na mfumo thabiti wenye kuleta maendeleo. Hii ni kutokana na athari tulizozipata wakati wa ukoloni mkongwe (Classical Colonialism) na Ukoloni Mamboleo, Vita ya Kagera na Maanguko ya kimataifa ya Uchumi. Hali hii iliathiri shughuli  za maendeleo kutokufanikiuwa kwa kiwango cha juu. Tanzania ilipitia kipindi kigumu kiuchumi na vita mwaka 1977 mpaka 1979 ambapo ilipelekea athari zaidi kiuchumi hadi miaka ya 1980 ambapo Tanzania ililazimika kukaribia soko huria ili kujenga uchumi. Miaka ya 1990 mpaka miaka ya 2000 Tanzania imesonga mbele kiamendeleo kutokana na juhudi mbali mbali marais ambao wamekuwa wakifanya katika vipindi tofauti vya uongozi wao ambapo Nyerere kutoka 1962 mpaka 1985, Mwinyi kutoka 1985 mpaka 1995, Mkapa kutoka mwaka 1995 mpaka 2005 na kwa sasa tuna Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alianza uongozi kama Rais kuanzia mwaka 2005 mpaka 2015.

3.   MAENDELEO WAKATI WA AWAMU YA NNE CHINI YA UONGOZI WA JAKAYA KIKWETE

Akiwa na dhamira ya kuhakikisha kwamba kila mtanzania anapata fursa sawa katika utumizi wa rasilimali asili na watu zilizopo ili kumjengea uwezo kila mtanzania kufikia kiwango cha maisha bora, Mh. Kikwete alinuia kuboresha maeneo ya msingi yatayowapeleka watanzania katika kilele cha “MAISHA BORA”. Ili kuijenga barabara ya kuelekea katika kilele hiki, awmu ya nne ya serikali yake ilitia mkazo katika maeneo kadhaa kama ifuatavyo:

a)    Kukuza utawala bora.

Mheshimiwa Rais, ni dhahiri kuwa kiwango cha utawala bora katika nchi yetu kimezidi kuimarika siku baada ya siku tena kwa ufanisi mkubwa tangu ulipoingia madarakani. Hilo linathibitika zaidi kwa kuaangalia maeneo mawili makubwa ambayo ni kupunguza urasimu katika shughuli mbalimbali za kiserikali ili kurahishisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi. Mashirika mbalimbali duniani yamekuwa yakitambua mchango wako na kukuwezesha kutunukiwa nishani mbalimbali ambazo hakika ulistahili, kama wasemavyo wahenga “ chanda chema huvikwa pete”

Kutokana na uongozi wako mahiri, Tanzania imepata mafanikio katika nyanja za demokrasia na utawala bora kama ambavyo Mpango wa Afrika wa Kujitathmini katika Utawala Bora (APRM) umebainisha kwamba Tanzania ni kati ya nchi zinazofanya vizuri kwenye eneo la utawala bora.  

 Tanzania imefikia katika kuridhia na kutekeleza mchakato wa Kujitathmini katika Utawala bora kwa nchi za Afrika (APRM) kuwa ni kuwashirikisha wananchi kutoa maoni yao kuhusu hali ya utawala bora nchini na serikali kuruhusu wataalamu wa utawala bora kutoka nchi wanachama kuja nchini kuhakiki mchakato huo. 
Ni ukweli kuwa APRM ni mpango ulioasisiwa Machi 9, mwaka 2013 na wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU)  ambapo Mheshimiwa rais ulikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Tanzania inatoa fursa ya kujipima na kujua mwenendo wa serikali na madereva wa utekelezaji (Viongozi wa serikali)
Tanzania kwa sasa ni miongoni mwa nchi 34 kati ya 54 za AU zilizokwishajiunga na mpango huu, ikiwa imejiunga tangu mwaka mwaka 2004. 
Suala la elimu.

Elimu ni nyenzo ya msingi katika jitihada za kujenga uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea na kuwawezesha kiuchumi wananchi. Uchumi wa kisasa unahitaji watenda kazi wenye maarifa yanayohusu kanuni na maarifa ya kumudu vitendea kazi vya aina mbalimbali.
Wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu vilivyopo nchini Tanzania waliongezeka kutoka 55,296 mwaka 2005/2006 hadi 118,000mwaka 2009/2010.Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka vyuo vikuu 23 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo 31 mwaka 2010.

Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kina wanafunzi 17,282

Wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka 493,636 hadi 999,070 huku idadi ya wanafunzi wanaogharamiwa na serikali toka familia zenye kipato duni ikiongezeka toka 16,345 hadi 58,843. Ongezeko hili ni kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2009. Pia Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka wanafunzi 638,591 hadi wanafunzi 889,363.
Tanzania imeweza kupiga hatua kubwa kwenye utaoji elimu kwa wananchi wake. Kwa kupitia(Mpango Wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi) MMEM, MMES na MEMKWA; watoto wengi wa Kitanzania wamepata fursa ya kujiunga na elimu ya msingi na sekondari. Hadi mwaka 2010 zaidi ya watoto milioni 8 (ambao ni zaidi ya 90% ya uandikishaji halisi) wameandikishwa shule za msingi na zaidi ya wanafunzi 1, 638, 699 wako sekondari.
Idadi ya shule na walimu imeongezeka maradufu. Hadi mwaka 2010 shule za sekondari zimeongezeka kutoka shule 937 na kufikia idadi ya 4,2663 mwaka 2010. Walimu nao wameajiriwa kwa idadi kubwa ili kusaidia mchakato wa kuwapatia watoto elimu. Kwa mfano, hadi mwaka 2010 idadi ya walimu wa shule za msingi na sekondari imefikia walimu 206, 3734 kutoka idadi ya walimu 54,869 mwaka 2001. Ongezeko hili limechangiwa na ongezeko kubwa la wanafunzi kwa kuanzia miaka ya 2001 hadi 2010.(tazama jedwali na 1). Hii ni dhahiri kuwa fursa za elimu kwa wote zimeongezeka nchini, na hatuna budi kuipongeza serikali chini ya Rais Jakaya Kikwete na wadau wa elimu kwa jitihada hizo.
Mafanikio katika sekta ya Afya
Mheshimiwa rais, tunapenda kukupongeza kwa kiasi kikubwa kwa jitihada zako katika sekta hii muhimu katika taifa letu. Wote tunafahamu maradhi ni moja kati ya maadui wakubwa ambao wanalisonga taifa letu  toka tupate uhuru.
Ni dhahiri kuwa tangu ulivyoingia madarakani umekuwa ukipambana kwa dhati ili kuhakikisha mapambano juu ya maradhi yanapungua kwa kiasi kikubwa. Wote ni mashahidi kwamba umepigania sana afya ya mama na mtoto kwa lengo moja kuu ambalo lilikuwa ni kupunguza vifo vya kina mama wajawazito pamoja na watoto  kwani hicho kimekuwa ni kilio kikubwa na tatizo kubwa ambalo linazikabili nchi zinazoendelea, kuna msemo usemao ukimsaidia mwamke basi umeokoa jamii nzima, hivyo basi ni dhahiri kuwa kwa nia yako hiyo umefanikiwa kuokoa jamii kubwa sana ya watanzaia wa kizazi kijacho.
Mheshimiwa Rais, umechangia kwa kiasi kikubwa kupambana na ugonjwa wa Malaria ambao umekuwa tishio sio tu Tanzania bali hata Afrika kwa ujumla lakini kwa jitihada zako za dhati kabisa toka moyoni ulikuwa muhamasishaji namba moja katika kupiga vita ugonjwa huu. Ni ukweli usiopingika kampeni mbalimbali kama vile “zinduka”  na zingine ambazo zilibeba dhana ya kuhamasisha jamii kutumia chandarua zimekuwa na mchango mkubwa sana katika jamii yetu.
Mheshimiwa Rais, vilevile umetoa mchango mkubwa sana katika vita dhidi ya ugonjwa hatari kabisa wa ukimwi kwani wakati unaingia madarakani ugonjwa huu ulikuwa ni tishio sana lakini kwa jitihada zako  umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizi kama ambavyo takwimu za tume ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) za mwaka 2014 zinatuonesha maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi nchini yamepungua hadi kufikia asilimia 5.1 kwa mwaka 2011/2012  ambapo asilimia 6.2 ni wanawake na asilimia 3.8 ni wanaume.
Mheshimiwa Rais, katika awamu zako mpaka sasa umejitahidi kwa kiasi  kikubwa Katika kuyaendeleza makundi mbali mbali ya kijamii,kwa namna moja ama nyingine, na katika hilo kuna mafanikio ya moja kwa moja ambayo yanonekana kama vile
Wanawake.           
 Hatua ya kurekebisha sheria zinazowabagua na
kuwadhalilisha wanawake katika usawa na maslahi yao imetekelezwa. Sheria ya makosa ya kujamiiana na sheria ya kuwalinda, wajane, zimerekebishwa na Sera ya Hifadhi na Maendeleo ya Wanawake, ziliboreshwa na kusimamiwa kwa kiwango stahiki kwa mfano uanzishwaji wa BENKI YA WANAWAKE pamoja na utoaji wa mikopo mbalimbali mfano mkopo kwa watu wa chini maarufu kama “MABILIONI YA JK”. Pamoja na miradi maalum wa kuinua kipato cha wanawake ili kupunguza ajira mbaya kwa watoto umeanzishwa.
Pia idadi ya wanawake katika nafasi  mbalimbali za juu za uongozi imeongezeka katika kipindi cha 2010-215 kwa mfano nafasi ya spika wa Bunge ambayo kwa sasa anahodhi mwanamke mheshimiwa Anne Makinda.... takwimu zinaonyesha katika kipindi cha uongozi wako nafasi za wanawake bungeni ni...... ambayo ni sawa na asilimia.... ukilinganisha na mwaka....pia hata katika bunge la katiba linaloendelea idadi ya wanawake ni... ..
Walemavu
Ili kulinda na kusimamia haki, usawa na maendeleo ya watu wenye ulemavu, Baraza la Taifa la Maendeleo ya Watu wenye Ulemavu, limeanzishwa chini ya uongozi wa Afisi ya Waziri Kiongozi. Aidha, Sera ya Walemavu imepitishwa na rasimu ya awali ya Sheria ya Walemavu imekamilika.
Hatua za kuelimisha jamii juu ya masuala mbali mbali ya kuwaendeleza watu wenye ulemavu, zimetekelezwa. Jumla ya watu 219 wenye ulemavu wamepatiwa mafunzo ya uendeshaji wa biashara ndogo ndogo Unguja na Pemba pamoja na kupatiwa mkopo wa kujiendeleza. Watu 193 wenye ulemavu wa kutosikia (viziwi)
wamepatiwa mafunzo ya lugha ya ishara.
Miundo mbinu
Kipindi cha miaka kumi iliyopita cha 2000 – 2010 tumeshuhudia kuwepo kwa
ujenzi mkubwa wa miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege na madaraja nchini. Miradi yote ya ujenzi ambayo haikukamilishwa kati ya 2000 – 2005 imekamilishwa kati ya 2005 – 2010 na kuanzishwa ujenzi wa miradi mipya kitakwimu, ujenzi wa miradi 15 kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu wa Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010. Aidha, ujenzi ambao unaendelea ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km. 2,536.4 na wakati huo huo miradi 7 ya barabara yenye jumla ya Km. 1,562 inaendelea kufanyiwa upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi. Hiki ni kielelezo dhahiri cha mafanikio makubwa ambayo yameiweka nchi yetu katika chati ya kuwa na miundombinu ya kisasa ya barabara.  Mwelekeo wa Sera za  serikali yako  katika miaka ya 2010 hadi 2020 umeainisha jukumu kubwa la nchi yetu katika kipindi hiki ni kutekeleza lengo la Dira 2025 la kuleta mapinduzi ya uchumi yatakayoitoa nchi kutoka kwenye dimbwi la uchumi ulio nyuma na tegemezi na kuiingiza katika mkondo wa uchumi wa kisasa wa taifa linalojitegemea.
Dhana ya Kujenga Uchumi wa Kisasa inalenga katika modenaizesheni ya uchumi.
Modenaizesheni kimsingi ni kuongeza maarifa na matumizi ya sayansi na teknolojia
katika sekta za uzalishaji. Modenaizesheni ya uchumi inalenga katika kuongeza
uzalishaji, ufanisi na tija katika uchumi hususan katika kilimo, ufugaji, uvuvi na
viwanda.
Mapinduzi ya Kilimo
Kilimo ndio msingi wa uchumi wa kisasa na njia sahihi ya kuutokomeza
umasikini.
Mheshimiwa rais umekuwa muumini wa dhati kwamba kilimo cha kisasa
kinachotumia Kanuni na zana bora za kilimo ndio ufunguo wa maendeleo ya
uchumi wa nchi yetu. Kilimo cha kisasa kina uwezo wa kutoa mazao mengi zaidi
kutoka kila ekari iliyolimwa. Kwa nchi yetu, ziada hiyo ya mazao ina faida kubwa
zifuatazo:-
(a) Kuipatia kila familia, kijiji na Taifa chakula cha kutosha ili kukomesha njaa.
(b) Kulipatia Taifa mavuno mengi ya kuuza ili kupata fedha za kigeni kwa ajili
ya maendeleo ya nchi.
(c) Ziada ya mazao huunda mazingira muafaka ya kuanzishwa viwanda vya
usindikaji na utengenezaji wa bidhaa za viwandani.
(d) Familia yenye ziada ya mazao huutokomeza umaskini kwa kuuza ziada
hiyo kwenye soko na kupata fedha za kujiletea maendeleo.
32. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ya utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2005-
2010, Serikali zetu zilichukua hatua kubwa katika kukipatia kilimo mwelekeo wa
kisasa ili kiondokane na zana duni, mashamba madogo, kutozingatia kanuni bora
za kilimo na kuridhika na mavuno ya kujikimu.
Mheshimiwa Rais, kwa heshima na taadhima tunapenda kukupongeza kwa dhati kwa kuanzisha mchakato wa Katiba mpya licha ya changamoto zilizojitokeza katika mchakato huo. Sote tunatambua nia yako ya dhati kuhakikisha taifa letu linapata katiba mpya kabla hujamaliza awamu yako ya pili ya uongozi hapo mwakani. Tunakusihi mchakato huu usiwe chanzo cha machafuko nchini mwetu bali maridhiano ya kisiasa yawe ndio msingi mkuu wa kupatikana kwa katiba itakayolivusha taifa letu kwa miaka mingi ijayo. Mwisho tunakutakia safari njema na mafanikio tele katika kutekeleza majukumu yako.
4.   CHANGAMOTO

a)    Kushuka kwa thamani ya shilingi

Shilingi ya Tanzania imekuwa haijatengamaa kwa vipindi tofauti tofauti ukilinganisha na Dola ya Kimarekani. Hali hii haijawa chachu katika juhudi za kimaendeleo zinazofanyika. Katika suala la kushuka kwa thamani ya shilingi, Serikali inatakiwa kujenga uchumi imara uliojengeka kwenye shilingi iliyoimara ukilinganisha na Dola ya Kimarekani

b)   Bajeti isiyotosheleza mahitaji

Bajeti ya Tanzania imekua isiyojitosheleza hasa kwa kuwa ni bajeti  tegemezi. hii imesasababisha mambo mengi kukwama.  wahisani wengi wamekua hawaleti pesa kwa wakati au kuleta fedha kwa masharti magumu yanaitesa nchi. Vyanzo vingi vya mapato vimekua visivyotosheleza na hivyo kupelekea bajeti ya maendeleo kuwa finyu ukilinganisha na mahitaji.       Katika suala hili  tunaishauri, Serikali ibuni vyanzo vipya na vya mbadala vya mapato ili kukusanya fedha ya kutosha itakayotoshereza mahitaji ya kibajeti

c)    Rushwa na ufisadi,

hili ni tatizo na tishio katika maedeleo ya Tanzania, viongozi wengi katika sekta mbalimbali Serikalini na hata sekta binafsi wamekuwa si waaminifu tena. Wamekuwa wakidai rushwa za aina tofauti au kufanya ufisadi, ubadhirfu wa fedha na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa kasi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

d)    Kushuka kwa uzalendo

Watanzania wa sasa si wa zamani. Zamani kulikuwa na misingi ya kimaadili na mafunzo iliyopelekea watanzania wengi kuipenda nchi yao na hivyo kupelekea kuwa wazalendo. Hali si hivyo tena kwa sasa, hii ni kutokana na kuibuka kwa changamoto mbalimbali za sayansi na teknolojia hivyo kumepelekea watu kuwa wabinafsi zaidi kuliko kujali masuala yanayohusu watanzania kwa jumla.

5.   HITIMISHO

          Mwisho kabisa mheshimiwa Rais, tunapenda kutoa pongezi zetu za dhati kwa kutunukiwa nishani mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani ikiwa ni ishara ya wao kutambua mchango wake baadhi ya nishani hizo ni kama Nishani Ubora wa Lulu ya Afrika (Bwana tukufu) Julai 2007 Nishani ya Hilali Kijani ya Komori Machi 2009,Nishani ya Abdulaziz Al Saud ,Aprili 2009,Nishani ya Ubora  Novemba 2009 ,Nishani ya Oman , Oktoba 2012 pamoja na tuzo za hivi karibuni za Tuzo la Nyota wa Demokrasia Afrika  2014 – Icon of Democracy Award Winner for 2014 in Africa
         Wewe ni kioo kwetu kama vijana na wapiganaji wengine wote, tutakufanya mwenye tabasamu siku zote kwa kuishi uvumilivu wako wa kisiasa na kiumbe kinachopenda mwafaka pale maslahiya kitaifa yanapotamalaki.
Wenu Mtiifu,
 Loveness Mamuya – Kada Mzalendo CCM Marekani

MANGULA AFUNGUA OFISI MPYA YA CCM-CHATO

$
0
0


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula katikati akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Ofisi ya CCM wilaya ya Chato. Wengine katika picha ni Mbunge wa Chato Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Geita Said Magalula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula kulia mara baada ya kumpokea katika kata ya Buseresere Mkoani Geita. Kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita ndugu Joseph Msukuma
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula juu ya gari akihutubia mamia ya wakazi wa Buseresere mara baada ya kuwasili katika eneo hilo.
Wananchi wa Buseresere wakimsiliza Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipopita kwenda kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Mangula.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akisalimiana na baadhi ya wananchama wa CCM katika kata ya Bwanga wilayani Chato mara baada ya kusimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili ya Ufunguzi wa Ofisi Mpya ya CCM wilaya ya Chato.
Taswira ya Jengo jipya la Ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Chato ambalo ilikuwa ni ahadi ya Mbunge wa Chato ambaye pia ni waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akihutubia wananchi wa Bwanga waliofika kumsalimia wakati akiwa njiani kuelekea Chato ambapo alizindua jingo jipya la Ofisi hiyo ya kisasa.
Kijana wa Kikundi cha Ngoma cha Chato akionyesha umahiri wake wa kuzungusha ringi la Tairi la baiskeli kwenye mboni yake ya jicho hali iliyowashangaza wananchi wengi waliofika.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kulia akifurahia jambo pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara Mhe. Philip Japhet Mangula akivuta utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Chato ambayo ilikua ahadi ya Mbunge wa Jimbo hilo.

TAIFA STARS, BENIN KUKIPIGA JIJINI DAR OKTOBA 12

$
0
0

 Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inashuka uwanjani Oktoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Programu ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya mechi hiyo itatangazwa baadaye na Kocha Mkuu Mart Nooij.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaendelea na taratibu nyingine kwa ajili ya mechi hiyo ikiwemo usafiri wa Benin kuja nchini, ambapo timu hiyo inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Oktoba 10 mwaka huu ikiwa na msafara wa watu 28.

Pambano la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha upendo kati ya viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu.

Wakati huo huo, kutokana na mechi hiyo ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inafanyiwa marekebisho madogo, na marekebisho hayo yatatangazwa kesho (Septemba 26 mwaka huu).

RAIS MALINZI KUFUNGA KOZI YA WANAWAKE

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatarajia kufunga mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara.

Hafla ya kufunga mafunzo hayo itafanyika kesho (Septemba 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Mafunzo hayo ya siku tano yalishirikisha viongozi 34 wakiwemo baadhi ya waandishi wa habari na Meneja wa Twiga Stars, na yaliendeshwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Henry Tandau.

Wafuasi wa Boko Haram wajisalimisha

$
0
0

http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/375/amz/worldservice/live/assets/images/2014/09/25/140925043609_boko_haram_304x171_afp_nocredit.jpg
Wanamgambo wa Boko Haram
Jeshi nchini Nigeria limesema zaidi ya wafuasi 260 wa Boko Haram wamejisalimisha Kaskazini mwa nchi hiyo. Jeshi hilo limesema katika mapambano limemuua mtu mmoja ambaye huwa anaonekana kwenye picha za video za propaganda za Boko haram akijidai kuwa Kiongozi wa wa kundi hilo, Abubakar Shekau.
Jeshi lilisema kuwa wapiganaji 135 walijisalimisha wakiwa na silaha zao katika eneo la Biu , jimbo la Borno siku ya Jumanne. Liliongeza kuwa wengine 133 walijisalimisha Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini Lagos Will Ross anasema kuwa ni vigumu kuthibitisha madai hayo ya jeshi.
Mwaka jana jeshi lilisema kuwa Shekau huenda aliuawa , lakini halikutoa thibitisho lolote. Hata hivyo ikiwa ni kweli kuwa wapiganaji hao wamejisalisha basi huenda ni ushindi kwa jeshi la Nigeria katika vita vyake dhidi ya Boko Haram.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kuwa majuma ya hivi karibuni Boko Haram imeshindwa kwa kiasi kikubwa wakati walipokuwa wakipambana kudhibiti eneo karibu na mji wa Maiduguri ambalo ni ngome yake.
Jeshi limesema wafuasi 135 wa Boko Haram wamejisalimisha wakiwa na silaha zao katika majimbo ya Biu na Borno,halikadhalika wafuasi wengine 133 wanahojiwa. Kwingineko , Rais wa Nigeria,Goodluck Jonathan amesema kuwa zaidi ya watu 13,000 waliuawa katika miaka mitano ya kwanza ya harakati za Boko Haram nchini humo.
Rais Jonathan alisema hayo katika hotuba yake katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Jumatano. Rais Jonathan pia alisisitiza kuwa juhudi zinafanywa kuwaokoa wasichana wa Chibok.Chanzo BBC swahili
Viewing all 16721 articles
Browse latest View live




Latest Images