Quantcast
Channel: EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Viewing all 16721 articles
Browse latest View live

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA MHESHIMIWA DKT. WILLIAM AUGUSTAO MGIMWA (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NAMATUMIZI KWA MWAKA 2013/2014 HII HAPA

$
0
0
 
 Waziri wa Fedha Dk William Agustao Mgimwa
----
       

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU PINDA BUNGENI DODOMA

$
0
0

 


 
IMG_0689
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Seriklai za Mitaa, Hawa Ghasia kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Juni 13, 2013. (Picha naOfisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0706
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi kwenye viwanja vya Bunge Mjini dodoma Juni 13, 2013. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0753
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizunguma na Wabunge Lolesia Bukwimba wa Busanda (katikati) na Felisita Bura wa Viti Maalum kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni13, 2013. (Picha na Ofisi yaWairi Mkuu

IMG_0725
Wabunge Batrice Shelukindo wa Kilindi (kushoto) ana Aza Hilal wa Viti Maalum wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Juni 13, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MSANII WA HIP HOP LANGA AFARIKI DUNIA .... UTHIBITISHO WA KIFO CHAKE HUU HAPA

$
0
0





Langa Kileo (msanii wa Hip Hop Tanzania, pichani)

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba msanii Langa amefariki dunia..


Habari zinadai kuwa , Msanii huyu alikumbwa na Malaria kali sana hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili jana.
UTHIBITISHO TOKA KWA AFISA UUGUZI HOSPITALI YA MUHIMBILI :
Aminiel Aligaesha ambae ni Afisa Uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili amethibitisha kwamba msanii Langa amefariki dunia June 13 2013 saa kumi na moja jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo toka juzi jioni ambapo kutokana na sababu za kimaadili kwenye tiba, Muhimbili hospitali hawawezi kusema rapper huyu alikua anaumwa nini bali ndugu ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Kwenye maelezo aliyoyatoa kwa millardayo.com Aminiel amesema Marehemu Langa alipokelewa kwenye idara ya wagonjwa wa magonjwa ya dharura usiku wa kuamkia jana na kupatiwa huduma ambapo leo June 13 2013 ndio alihamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa Mahututi na baadae kufariki dunia.

KICHANGA CHA SIKU CHAOKOTWA JALALANI KIKIWA KIMESHAFARIKI

$
0
0

SONY DSC
Wakazi wa eneo la magomeni zilipovunjwa nyumba za( KOTA) jijini Dar es salaam leo wakishuudia mototo mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja akiwa ametupwa na kufariki dunia katika eneo hilo na mtu asiyefaamika.
SONY DSCSONY DSC
Askari polisi wa kituo cha magomeni usalama wakiwa  katika eneo ambalo ametupwa mtoto mchanga akiwa amefariki kwa ajili yakumchukua kumpeleka sehemu husika
SONY DSC
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)

WABUNGE WAWA MBOGO, WAIRARUA BAJETI YA SERIKALI 2013-2014 ..... HAYA HAPA NI MAONI YAO

$
0
0
BAADHI ya wabunge wametoa maoni yao kuhusiana na Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/14, yakionekana kung’ata na kupuliza. Hali hiyo, ilitokana na wabunge wengi wa CCM kudai bajeti hiyo ni nzuri na imegusa kila idara, huku wapinzani wakidai haina jipya kutokana na kushindwa kubuni vyanzo vipya vya mapato.

Akitoa maoni, Kingozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Chadema), alisema hakuna jambo la kushangilia katika bajeti hiyo, kwa kuwa utaratibu ni uleule.

Alisema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), bado imeng’ang’ania kuongeza mapato katika soda, bia na sigara na kuacha sekta ambazo zinauwezo mkubwa wa kuongeza mapato ya Serikali.

“Vipo vyanzo vya mapato kama vile madini, gesi na maliasili lakini mchango wake ni mdogo.

“Nashangaa wabunge wa CCM wanaishangilia bajeti wakati inakwenda kuwaumiza wananchi, kutokana na kupandisha bei ya mafuta.

“Bajeti hii, pia haijaonyesha msisitizo wowote wa kubana matumizi ya Serikali, matumizi ya Serikali bado ni makubwa.

“Na jambo kubwa la kujifunza ni kwamba, Serikali haina utaratibu wa kutekeleza bajeti yake, kilichoelezwa hapa bungeni na utekelezaji wake itakuwa ni tofauti,” alisema Mbowe.

Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi) naye aliikosoa Serikali kuongeza kodi kwa bia na vinywaji vingine, huku ikishindwa kutafuta vyanzo vingine vya mapato.

“Kwa mfano katika sekta ya bahari kuu, tunaweza kukusanya zaidi ya bilioni 821, badala ya kuongeza kodi kwenye bia.

“Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika, hakukuwa na tija yoyote kwani baada ya Serikali kuongeza kodi ya bia katika bajeti ya mwaka jana, watu wengi walihamia katika matumizi ya pombe za kienyeji ambazo kwa kiasi kikubwa zinaathiri nguvu za kiume,” alisema Mbatia.

Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP) alisema bajeti hii ni ya kihistoria tangu Tanzania ipate uhuru, kwa kuwa mwaka huu wabunge wameshiriki kuipitia pamoja na kuomba kuongezwa fedha katika baadhi ya bajeti za wizara.

“Tumeshuhudia leo Serikali imeongeza zaidi ya Sh bilioni 500 zilizoombwa na wabunge, zamani fursa hii haikuwepo,” alisema Cheyo.



Mbunge wa Igunga, Dk. Dalay Kafumu (CCM), aliisifia bajeti hiyo kwamba ni nzuri kwa kuwa wabunge walipata fursa ya kuipitia na hivyo kusababisha marekebisho mengi kufanyika.

Mbunge wa Viti Maalum, Magreth Sitta (CCM), alisema amepokea bajeti hiyo kwa matumaini makubwa hasa katika kipengele cha mapato ya simu, ambapo mapato hayo yataelekezwa katika sekta ya elimu.

Mbunge wa kuteuliwa, Zakhia Meghji (CCM) amezungumzia kuhusu Sera ya Fedha ambapo alisema wabunge waliipigia mno kelele sera hiyo hususan katika suala la riba kubwa kwa sekta ndogo.

Alisema kuweka sera maalum ya fedha, itawasaidia wananchi waliojiunga kwenye vikoba na SACCO's kuanzisha benki zao wenyewe ambazo zitatoza riba kidogo.

Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (CCM) alipongeza mfumo mpya wa kujadili bajeti, kwa kuwa wabunge wamepata fursa ya kujadiliana na Serikali na kuongeza fedha katika maeneo yaliyolalamikiwa kuwa na pungufu.

“Mfumo huu umesaidia kufanyiwa marekebisho katika baadhi ya maeneo ikiwemo katika sekta muhimu za umeme na maji, hivyo wananchi wengi watanufaika hususan wa maeneo ya pembezoni,” alisema.

Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alisema bajeti hiyo haina jipya kwani imebaki kupandisha kodi ya bia na sigara na kuacha maeneo muhimu yanayoweza kuliingizia taifa mapato.

Mbunge huyo pia alihoji sababu za Serikali kupata kigugumizi katika kupiga marufuku matumizi ya magari ya kifahari kama vile mashangingi, ili kubana matumizi ya Serikali.

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema) mbali na kuzungumzia utaratibu uleule wa kuongeza kodi katika bia na soda, alisema pia misamaha mingi ya kodi bado haijaondolewa na utaratibu wa kuyabana makampuni makubwa yalipe kodi haujawekwa bayana.

“Pia Serikali imeongeza kodi ya petroli na dizeli za aina tatu kwa wakati mmoja, hali itakayochangia ongezeko la gharama za usafiri, usafirishaji na uzalishaji na hivyo kuongeza mfumuko wa bei na gharama za maisha kwa wananchi.

“Serikali haijaja na mkakati madhubuti wa kupunguza gharama zisizo za lazima na kudhibiti ufisadi kwenye manunuzi,” alisema Mnyika.


MTANZANIA

WAZIRI MKUU PINDA AFUNGUA SEMINA YA YA MTANDAO WA WABUNGE APNAC

$
0
0

 

IMG_0909
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akionyesha Tuzo ya heshima aliyopewa Rais Jakaya   Kikwete  na Mtandao wa wabunge  wa mabunge wa Afrika wa kupambana na rushwa APNAC ili kutambua mchango wake katika kupambana na rushwa. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye semina na SPNAC iliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Afrian Dream mjini Dodoma Juni 14, 2013.  Kushoto ni Spika wa Bunge Anne Makinda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0923
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Spika wa Bunge Anne Makinda (katikati)  na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Gerge Mkuchika baada ya kufungua semina ya Mtandao wa wabunge  wa mabunge wa Afrika wa kupambana na rushwa APNAC  iliyofunguliwa na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Afrian Dream mjini Dodoma Juni 14, 2013.  Kushoto ni Spika wa Bunge Anne Makinda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0963
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiteta na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika baada ya kufungua semiana ya Mtandao wa Wabunge wa  Afrika waanaopambana na Rushwa APNAC kwenye ukumbi wa Afrian Dream mjini Dodoma Juni 14, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0979
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Jaji Kiongozi, Fakih  Jundu (kakatikati) na Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa baada ya kufungua semiana ya Mtandao wa Wabunge wa  Afrika waanaopambana na Rushwa APNAC kwenye ukumbi wa Afrian Dream mjini Dodoma Juni 14, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0986
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Naibu Waziri wa Habari , Vijana na Michezo, Amos Makala kwenye viwanja vya Hoteli ya African Dream mjini Dodoma Juni 14, 2013. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TCU YAPIGA STOP TIU KUTOA SHAHADA

$
0
0

 



imagesNA BELINDA KWEKA,MAELEZO-DAR ES SALAAM
Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) imekifunga Chuo Kikuu cha Kimataifa Tanzania(Tanzania International University -TIU) kudahili wanafunzi  ngazi ya shahada kutokana na  kutotimiza masharti na vigezo vinavyohitajika na Tume hiyo ili kuendesha mafunzo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari Afisa habari mwandamizi wa Tume hiyo Edward Makaku,  (leo) jijini Dar es salaam amesema kuwa Chuo hicho kimefungwa kutokana na kutotimiza masharti ya kufundisha kozi ya shahada ikiwa ni pamoja na kukosa walimu wanaokidhi vigezo vya kufundisha ngazi hiyo.
 “Tunapenda kuwatangazia kuwa chuo hicho ni chuo kikuu binafsi na kimesajiliwa kuendesha mafunzo yake kwa leseni namba CR1/028 na imepitiwa na Tume ya vyuo vikuu na kuruhusiwa kutoa mafunzo yake kwa ngazi ya cheti, stashahada na kozi za muda mfupi lakini sio kwa ngazi ya shahada, naomba wananchi waelewe hili”, alisema Edward.
Aidha  Edward ameongeza kuwa mapema Aprili mwaka huu Tume ilitoa mwongozo kukitaka chuo hicho kusitisha  mafunzo yake katika ngazi ya shahada mpaka kitakapokidhi masharti na kupatiwa usajili.
“Napenda kutoa tahadhari kwa wananchi kutojiunga na chuo hicho kwa ngazi ya shahada kwani hakijakidhi vigezo vya kutoa shahada kama inavyotakiwa na Tume bali wanaweza kujiunga katika ngazi za cheti, stashahada na mafunzo ya muda mfupi”, ameongeza.
 Tume imeutaka uongozi wa  chuo hicho kuacha kudahili wanafunzi na kurudisha ada na gharama nyinginezo kwa walosajiliwa ngazi ya shahada.

SERIKALI SASA YARUHUSU SIMBA NA YANGA ZIENDE SUDAN KUCHEZA KAGAME

$
0
0

 

Mh Amos Makalla kushoto akiwa na Ofisa wa Executive Solutions, Waratibu wa Udhamini wa Simba na Yanga kutoka TBL, Michael Mukunza kulia  
 
Na Mahmoud Zubeiry wa Bin Zubeiry
 
SERIKALI imeziruhusu klabu za Simba SC, Yanga SC za Dar es Salaam na Super Falcons ya Zanzibar kwenda Sudan kushiriki michuano ya Klabu Buingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makalla amefanya Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma asubuhi ya leo kusema wameruhusu klabu hizo ziende Sudan baada ya kuhakikishiwa na Serikali ya nchi hiyo kwamba itatoa ulinzi wa kutosha dhidi ya timu za Tanzania.
Makalla amesema wameandikiwa barua na Serikali ya Sudan ikiwahakikishia kwamba timu za Tanzania zitapewa ulinzi mkubwa zisiathirike na machafuko yanayoedelea Sudan.
Kufuatia tamko la Serikali kuziruhusu klabu hizo sasa ziende Sudan, sasa ni juu yao ya klabu hizo kuamua kwenda au kutokwenda.
Lakini Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Mkenya Nicholas Musonye amekwshatishia atazichukulia hatua kali klabu hizo zisipokwenda.
Juzi Serikali kupitia Makalla ilitoa tamko la kuzuia klabu za Tanzania kutokwenda Sudan kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo. 
Kufuatia tamko hilo, jana Yanga, ambao ni mabingwa watetezi kwa miaka miwili mfululizo, walitangaza kuvunja kambi yao hadi wiki mbili baadaye, wakati Kombe la Kagame linaanza kutimua vumbi Juni 18, mwaka huu.
Yanga wamepangwa Kundi C katika michuano hiyo pamoja na Ports ya Djibouti, Express ya Uganda na Vital 'O' ya Burundi, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC wamepangwa Kundi A pamoja na wenyeji El-Mereikh, Elman  ya Somalia na APR ya Rwanda.
Katika michuano hiyo inayotarajiwa kufikia tamati Julai 2, mwaka huu mjini Khartoum, Sudan, mabingwa wa Kenya, Tusker wamepangwa Kundi B pamoja na wenyeji wengine, Al-Hilal, Falcons ya Zanzibar, Al Ahly Shandy ya Sudan na Al-Nasir Juba ya Sudan Kusini.
Yanga wataanza kampeni zao za kutetea taji hilo Juni 20 kwa kumenyana na Express, wakati Simba SC itashuka dimbani Juni 21 kufungua dimba na El-Mereikh, na mechi zote zitachezwa Elfashar.

KIKOSI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UJANGILI TANAPA CHAHITIMU MAFUNZO RUAHA NATION PARK

$
0
0

 


 1Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akikagua gwaride la kikosi maalum cha kupambana na ujangili katika hifadhi za taifa wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika mbuga ya Ruaha kandokando ya mto Ruaha wakipewa mafunzo hayo na wakufunzi Martin Mthembu kutoka taasisi ya African Field Rager Training Services ya Afrika kusini, kikosi hicho maalum cha TANAPA kilikuwa na askari 20 wamehitimu mafunzo hayo askari 19 moja hakufanikiwa kumaliza mafunzo kwa sababu za kiafya, Kivutio kilikuwa kwa askari mwanamke pekee katika kikosi hicho Aikandaeli Lema ambaye aliweza kufanya mafunzo kwa kiwango cha juu bila kuwa na tofauti yoyote kiutendaji ya kijinsia ameza kufanya mafunzo yote magumu na kulenga shabaha kwa kiwango cha juu kabisa alimwelezea mkufunzi wa mafunzo hayo Martin Mthembu kutoka Afrika Kusini na akampa sifa na pongezi nyingi kwa uwezo wake kama mwanamke. 3Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akirejea meza kuu mara baada ya kukagua gwaride hilo katika ufungaji wa mafunzo hayo4Kikosi hicho kikitembea kusonga mbele tayari kwa kutoa heshimza zao kwa mgeni rasmi.6Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akipokea heshima kutoka kwa kikosi hicho wakati alipofunga mafunzo rasmi ya kukabiliana na ujangili katika hifadhi za taifa kulia ni Adam Swai Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Iringa na kushoto ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki.7Askari wahitimu wa kikosi hicho kushoto ni Frank Anthon Malema na Mwanamke pekee katika kikosi hicho Aikandaeli Lema wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo8Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo10Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo askari Frank Anthon Malema kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo na mhifadhi TANAPA Genes Shayo 11Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo askari Elisamehe Elisafi Mdeme kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA Martin Loiboki na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo na mhifadhi TANAPA Genes Shayo 12Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimpongeza John Kijazi baada ya kupokea cheti cha kuhitimu mafunzo hayo 13Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo.14Martin Mthembu Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka nchini Afrika Kusini akitoa maelezo kwa Allan Kijazi Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA wakati akikagua eneo maalum la kulenga shabaha katika ufungaji wa mafunzo hayo kulia ni Dr. Christopher Timbuka mhifadhi mkuu wa Ruaha Nation Park.15Askari maalum wa kikosi hicho cha kupambana na ujangili katika hifadhi za taifa wakionyesha moja ya kazi zao wakati wakitafuta majangili katika hifadhi hizo16Mmoja wa Askari wa kikosi hicho akilenga shabaha 17Mkufunzi wa Mafunzo hayo Martin Mthembu akielezea mafanikio ya kikosi hicho katika kulenga shabaha kwa mkurugenzi wa hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi wa pili kutoka kushoto wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi Martin Loiboki na wa kwanza kushoto ni Dr. Christopher Timbuka Mhifadhi Mkuu Ruaha Nation Park20Mkufunzi Martin Mthembu akielezea jinsi askari hao wanavyotakiwa kuwatafuta majangili huku wakiwa na maamuzi ya haraka bila kuchelewa na kutoua jangili ambaye hana madhara askari wa anatakiwa kufanya kazi yake kwa ufanisi lakini pia kulinda usalama wake yaani fanya kazi yako lakini rudi salama21Askari mwanamke pekee Aikande Lema akilenga shabaha huku mkufunzi huyo akiangalia22Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi naye akimshuhudia askari huyo23Askari Aikande Lema akirejea mara baada ya kumaliza kazi aliyotumwa na mwalimu wake kwa mafanikio katika kulenga shabaha.24Mto ruaha 25Mnyama tembo yuko hatarini kutoweka kutokana na majangili kuwauwa kwa wingi wakichukua pembe zake 
 27 
Twiga ni mojawapo ya wanyama ambao pia wanauliwa na majangili28Mhifadhi wa Ruaha Nation Park Paul Banga akitoa maelekezo kwa wahariri wa vyombo vya habari kabla ya kuingia mbugani jana kwa lengo la kujifunza utalii wa ndani na kujionea wanyama mbalimbali wanaopatikana katika hifadhi hiyo29Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika geti la kuingilia kwenye mbuga ya Ruaha Nation Park.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-RUAHA NATION PARK

KAULI MBALIMBALI ZA MASTAR WALIZOTOA KUFUATIA KIFO CHA MSANII LANGA HIZI HAPA

MFAHAMU VYEMA MAREHEMU LANGA KILEO 'LANGA'

$
0
0



Ni mtaalamu na mwanamuziki stadi wa Hip Hop nchini aliyeweka wazi kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.

 Ili kuonyesha anachukizwa, Langa alilieleza jarida moja la burudani kwamba anakusudia kuanzisha Taasisi ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya.

Alisema matumizi ya dawa hizo yaliathiri shughuli zake za muziki na hakuwa na jambo lolote endelevu katika muziki wake.

Kimuziki Langa alianzia kundi la Wakilisha akiwa na Witness Mwaijega na Sarah Kaisi, ambapo walikuwa washiriki wa mashindano ya muziki ya Cocacola Pop stars, yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.

Wakiwa na kundi hilo walifanikiwa kufyatua kibao cha ‘Hoi’, ambacho kiliteka wapenzi wa muziki.

Baadaye Sarah Kaisi (Shaa) alijitoa. Lakini Langa na Witness walifyatua kibao cha ‘No Chorus’.

Baada ya hapo Langa alifyatua kibao chake cha kwanza akiwa mwanamuziki binafsi, ‘Matawi ya Juu’ ambacho Dj John Dilinga (JD) aliwahi kuelezea ni moja ya kazi nzuri kutoka kwake, licha ya dosari za matumizi ya lugha.

Hata hivyo Langa alionyesha yeye ni bora na ana kipaji cha muziki. Amekuwa shujaa kwa kuendesha kampeni kali za kupinga matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana. Serikali inapaswa kusaidia juhudi zake pamoja.



Huyu ni mmoja wa matunda ya shindano la muziki la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004 ambalo washindi wake waliounda kundi la Wakilisha.  Mbali ya Langa, wengine ni Sarah Kaisi `Shaa’ na Witness Mwaijaga `Witness’. Huo ndio uliokuwa mwanzo wa kung’ara kisanii kwa wakali hao, ingawa kwa sasa kundi hilo limesambaratika, kila mmoja akitamba kivyake. 


Lakini kwa bahati mbaya, mmoja wao, Langa kwa miaka ya hivi karibuni hakusikika kabisa, jambo lililomlazimu mwandishi wa makala haya kumtafuta sababu za ukimya wake.



Haikuwa kazi rahisi, lakini hatimaye Langa alipatikana na bila kutafuna maneno alisema kwamba, alishindwa kufanya kazi baada ya kuwa `teja’ aliyekubuhu.


Yaani alizama katika matumizi ya dawa za kulevya kiasi cha kupoteza kabisa mwelekeo si wa kisanii pekee, bali hata kimaisha.


“Siyo siri, kilichokuwa kimenifikisha katika hali hiyo ni dawa za kulevya. Kwa miaka mitano nilitumia sana Cocaine, Heroin, bangi na pombe. Namshukuru Mungu sasa nimerejea katika hali yangu.

“Siamini kama nimenusurika kwa sababu madawa yalinitesa, nikafanya mengi ya ajabu yaliyoichukiza familia yangu na marafiki ikiwa pamoja na kuwa mwizi na mkabaji mitaani na nyakati za usiku,” anasema Langa ambaye kundi lao la Wakilisha lilitamba na nyimbo kama `Unaniacha Hoi’ na `Kiswanglish’.


Anaeleza kwamba, kwake hayo ndiyo aliyoyaona maisha yanayomfaa, akidai awali alikuwa amechoshwa kuishi kwa masharti kutoka kwa wazazi wake waliokuwa wanampa mwongozo wa maisha, lakini bila kujua akadhani `anachungwa’. 


Kwamba, umaarufu na ngekewa ya kuzishika pesa katika umri mdogo kupitia muziki vilimtia kiburi zaidi, na hivyo kuamua kujitenga kabisa na familia yake iliyomlea kwa mapenzi mazito.

“Niliamini naweza kujitegemea kupitia kazi yangu ya muziki, nikajichanganya mtaani,” anasema kijana huyo aliyetoa kibao chake cha kwanza, Matawi ya Juu mara baada ya kusambaratika kwa kundi la Wakilisha kutokana na kila mmoja kuamua kujitegemea kimuziki. Na kweli, Matawi ya Juu ilidhihirisha kuwa Langa ni moto wa kuotea mbali katika fani. Aliweza kusimama kwa miguu yake na kutikisa.


Mwenyewe anasema: “Jina hilo la Matawi ya Juu lilidhihirisha hivyo pale video ya kibao hicho ilipotajwa kuwania Tuzo za MTV Base kwa upande wa hapa Bongo miaka michache iliyopita, kisha kutwaa Tuzo ya Kisima nchini Kenya.



“Moto huo uliwafanya baadhi ya wasanii wakongwe katika gemu ya Bongo Fleva kunitafuta na kunipa majukumu ya kushiriki katika kazi zao, ikiwemo Chagua Moja ya Farid Kubanda `Fid Q’. 


“Baada ya kuona wakongwe wamekubali vitu vyangu na kuanza kunishirikisha…nikapata pia safari za nje ya nchi. Huko Nairobi (Kenya) niliweza kufanya kazi na vichwa vikali vinavyounda Kundi la Necessary Noise, Naaziz na Wyre (Kevin Wyre).


Anasema mafanikio hayo yalimtuma kufyatua albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la Langa, akiamini itampaisha zaidi kimaisha na kimuziki. Hata hivyo, mambo yalikwenda kinyume. Anasema alipoipeleka sokoni, wauzaji wakubwa waliigomea, hivyo kumpa wakati mgumu wa kuwaza na hatimaye kujikuta akiongeza kasi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Siyo siri, kugoma kwa albamu yangu sokoni kulichangia kasi ya kutumia dawa za kulevya…niliona ni njia pekee ya kuondoa mawazo kwa sababu kazi iligoma, na home (nyumbani) nilishaharibu.


Sikufanya tena kazi kwa umakini na kila kazi niliyoitia haikufanya vizuri….” Anasema kwamba, baada ya mambo kumwendea mrama, ndipo alipoanza kuiba vitu nyumbani kwao kwa lengo la kuviuza na inapotokea amekosa, alidiriki hata kupiga debe katika vituo vya mabasi ili mradi apate fedha za kununua `unga’. 


Haikuishia hapo, kwani anasema alijiingiza katika kundi la wahuni waliojihusisha na wizi na ujambazi. “Kwa ujumla nilipoteza mwelekeo. Maisha yangu yakawa ya kutembea na kisu kama kitendea kazi changu katika wizi,” anasema huku akitikisa kichwa kama ishara ya kujutia matendo aliyoyafanya kwa msukumo wa madawa ya kulevya. Anakumbuka akiwa mtumwa wa `unga’, aliingia katika mikasa kadhaa ikiwa pamoja na kupigana na polisi baada ya kunaswa na dawa hizo haramu. 


Katika wizi, chochote alichokikuta mbele yake kilikuwa halali. Anasema alikwapua vitu magengeni, madukani na hata magari yaliyoegesha vibaya alinyofoa vioo na mashine zinazosaidia kupandisha na kushusha vioo ndani ya gari. 


“Ni matukio ya aibu. Yanasikitisha…,” anasema Langa anayedokeza kwamba, akiwa mtumiaji wa `unga’, alikuwa anakutana na wasanii na watu wengine mashuhuri. Hata hivyo anakataa kuwataja, akidai ni siri yake. `Ufufuo’ wa Langa kutoka katika lindi la mateso ya dawa za kulevya ulipatikana kuanzia Machi mwaka huu, baada ya familia yake kumpeleka kijana wao kwa tiba maalumu ya kuachana na matumizi ya `madudu’ hayo. Na kweli, elimu imemwingia na kujikuta akirejea ufahamu wake wa kawaida.


Ametangaza kuachana na `unga’, pombe, sigara na badala yake amejikita zaidi katika mazoezi ya kurudisha mwili wake katika hali ya kawaida. Aidha, amekata shauri la kuirudia fani yake na tayari ana vitu vipya, Bombokiata na Mteja Aliyepata Nafuu.


Anasisitiza kwamba, kutokana na mateso aliyoyapata, anakusudia katika siku za baadaye afungue kituo chake cha tiba ya dawa za kulevya ili aweze kuwaokoa vijana wengine wanaoangamia kutokana na matumizi ya dawa hizo haramu zinazopigwa vita karibu kote duniani. “Nimenusurika, namshukuru Mungu.


Nami najipanga kutaka kuwasaidia wengine waachane na mateso ya dawa za kulevya. Pia nichukue fursa hii kuwaomba msamaha wote niliowakosea kwa namna moja ama nyingine wakati nikiwa `teja’,” anasema Langa, kijana mwenye umri wa miaka 25.


Je, historia ya maisha ya Langa ikoje? Anasema Desemba mwaka 1985 jijini Dar es Salaam akiwa tunda la wanandoa Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo. Alisoma Shule ya Msingi Olympio na Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam.


Hata hivyo, akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye Shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda. Baadaye alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma.


Huyo ndiye Langa Kileo msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye baada ya kulewa umaarufu na kujikita katika matumizi ya dawa za kulevya, ameibuka na kujutia `ujanja pori’, sasa akitaka kujiingiza katika kampeni ya kuwaokoa vijana wengine waliozama katika `unga’. Anakusudia pia kurudi darasani kujiendeleza na masomo ya elimu ya juu. Je, atafanikiwa? Kwa hakika, hili ni jambo la kusubiri na kuona.

LWAKATARE WA CHADEMA NDANI YA BIFU ZITO NA MTATIRO WA CUF

$
0
0


Jackson Odoyo, Dar es Salaam.
MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama Wilfred Lwakatare amejitokeza adharani na kumvaa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Julius Mtatiro kutokana na kauli yake aliyowahi kuitoa kwamba Lwakatare alipokuwa Chama Cha Wananchi (CUF) hakufundishwa ugaidi.

Lwakatare ambaye aliachiwa uhuru kwa dhamani hivi karibuni baada ya kukaa mahabusu kwa siku 92, alimshambulia Mtatiro katika waraka wake mrefu ambayo nakala yake imenaswa na mtandao wa Habarimpya.com, alisema kwam
ba hakuelewa maana ya maneo hayo ya Mtatiro aliyoyatoa mbele ya Waandishi wa Habari wakati akiwa mahabusu.

"Nikiwa Gerezani Segerea nilimshangaa sana ‘bwana mdogo’ Julius Mtatiro- alipozungumza kwenye vyombo vya habari kuwa ”Lwakatare akiwa CUF hatukumfundisha ugaidi.”

Sikumuelewa hayo maneno alikuwa na maana gani na alitumwa na nani"alisema Lwakatare na kuongeza.

"Kwanza sijui kipindi hicho nikiwa CUF yeye alikuwa wapi na sidhani kama kwa wakati huo alifikiria hata kujiunga na hiyo CUF.

Awaulize CUF ‘Original’ kama wapo, Lwakatare alikuwa ni nani ndani ya CUF".

Lwakatare katika wakaraka huo alifafanua kwamba hata siku moja haitatokea akabeza uzoefu na msingi wa kisiasa alioujenga ndani ya akili yake na nafsi yake kutoka CUF, na kwamba CUF ilimweka katika ramani ya kisiasa anayoitumia kutamba nayo hadi leo hii.

"CUF ilinijengea nguzo moja kubwa iliyonipaisha kisiasa na inayoendelea kunisaidia katika kazi niliyokabidhiwa Chadema ya ulinzi wa chama hadi leo, ambayo ni ujasiri, kujitoa kwa nafsi yangu na kwa akili zangu zote kuipigania na kuitafuta haki bila kuchoka na kutokukubali dhuluma na uonevu, haki huwa huletewi kwenye kisahani cha kikombe cha chai, haki hudaiwa na kutafutwa.

MBOWE,CHEYO WAIPONDA BAJETI

$
0
0

 


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ameiponda Bajeti ya Serikali kwa madai kuwa haina jipya na wala haina nia njema ya kupunguza umaskini kwa Mtanzania.
Kauli hiyo aliitoa jana, muda mfupi katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima baada ya kumalizika kusomwa kwa Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2013/14 iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa.
Mbowe alisema kuwa bajeti ambayo imesomwa na serikali
licha ya kushangiliwa na wabunge wa CCM haina makusudi ya kuwasaidia Watanzania ambao ni maskini na badala yake wamewatwisha mzigo kwa kupandisha bei ya mafuta.
“Tumekuwa tukishuhudia kila mwaka serikali inaweka kodi katika vinywaji pamoja na sigara lakini inashindwa kueleza ni kwa jinsi gani wanaweza kupata mapato kutoka katika rasilimali mbalimbali ambazo zipo nchini kama vile madini, utalii pamoja na vyanzo vingine vya mapato,” alisema Mbowe.
Mbali na hilo, Mbowe alisema serikali bado inaendelea kuwa na matumizi makubwa na hilo wanalifanya kwa makusudi huku wakiwakomoa wananchi ambao wana kipato kidogo kwa kupandisha ushuru wa magari pamoja na mafuta.
Naye Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), alisema kuwa pamoja na nyongeza kidogo ya mapato ya bajeti, serikali bado imeendeleza na utamaduni wa kuongeza bei kwa vyanzo vile vile vya pombe, sigara, mafuta na magari wakati vyanzo vinavyohusu rasilimali za nchi kama madini pamoja na makampuni makubwa, misamaha mingi bado haijaondolewa na mfumo wa kuyabana haujatangazwa.
Alisema kitendo cha serikali kuongeza kodi katika mafuta ya petroli na dizeli za aina tatu kwa wakati mmoja, kitachangia ongezeko la kupanda kwa gharama za maisha ikiwa ni pamoja na kupanda kwa nauli.
Alisema serikali haijaonesha mkakati madhubuti wa kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima katika bajeti ya sh trilioni 18.2 kwenye mapato na matumizi na asilimia 40 kupotea kutokana na matumizi mabaya kama ilivyo kuwa ikitokea katika miaka ya nyuma kutokana na serikali kuwa na tabia ya kufanya matumizi makubwa kuliko thamani ya fedha.
Kwa upande wake Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), alisema bajeti ya serikali bado haikuzingatia umaskini wa Watanzania na badala yake imekuwa bajeti ya kiushabiki.
Cheyo alisema kuna vyanzo vingi vya mapato ambavyo vingeweza kutumika kuliongezea taifa kipato kikubwa tofauti na kuongeza kodi katika vinywaji na ushuru wa magari.
Naye Mbunge wa Kigoma Kusini. David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alisema Bajeti ya Serikali haizungumzii ajira kwa vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa ajira.
Kwa upande wa viongozi wa dini katika Mkoa wa Dodoma, Askofu wa Kanda ya Kati katika Kanisa la PAG, Charels Kanyika, alisema licha ya bajeti kuonekana ina unafuu, serikali siku zote imekuwa ikisema mambo ambayo hayatekelezeki.
“Bajeti inaonesha uchumi umekua, lakini bado Watanzania wengi ni maskini, tena hawajui hata hatima ya mlo wao kwa siku. Kuwapandishia bei ya mafuta moja kwa moja ni kuendelea kuwakomesha,” alisema Askofu Kanyika.
Akizungumzia suala la bodaboda, alisema kuwaondolea ushuru ni jambo la kisiasa, kwani kutapunguza mapato ya taifa na kama wangetozwa angalau kiasi kidogo, wangeweza kuongeza pato la taifa.

POLISI MWINGINE WA KITUO CHA MAGOMENI ATIMULIWA KAZI BAADA YA KUPIGA PICHA ZA NUSU UCHI

$
0
0

 



POLISI wa kike wa Kituo cha Magomeni, jijini Dar es Salaam aliyejulikana kwa jina moja la Anisa, ametimuliwa kazi kwa madai ya kupiga picha ya utupu iliyosambaa mitandaoni.

Chanzo makini ndani ya jeshi hilo kilisema Anisa alifukuzwa kazi wiki iliyopita baada ya kuhojiwa na mabosi wake wa makao makuu ya jeshi hilo na kukiri kuwa picha hiyo ni yake.

“Anisa aliitwa makao makuu, mabosi wakamuonesha picha yake akiwa mtupu kitandani, akakiri ni yeye. Alijitetea eti alifanya hivyo kwa sababu siku ya tukio alikuwa amelewa sana,”kilisema chanzo.

Chanzo kiliendelea kudai kwamba baada ya afande huyo mwenyeji wa Tanga kukiri, viongozi wa jeshi hilo walimwambia amekiuka kanuni na kulidhalilisha jeshi hilo hivyo hataendelea kuwa mtumishi.

Picha ya afande huyo imeenea mitandaoni na kwenye baadhi ya simu za mikononi za watu kitendo kulicholifanya jeshi hilo kufanya uchunguzi na kubaini kuwa ni yake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina, Suleiman Kova alipoulizwa juzi alikiri kufukuzwa kwa askari huyo na kumtaka mwandishi wetu kufuatilia zaidi kwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura ambaye naye alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikiri.
‘‘Tunahitaji askari wenye maadili mema ndani ya jeshi letu, yule atakayefanya mambo bila kufuata kanuni na sheria hatua kali zitachukuliwa dhidi yake. Askari muda wote anatakiwa awe mfano bora kwa jamii,’’ alisema Afande Wambura.

Taarifa zaidi zinadai kwamba kwa sasa Anisa anaishi uraiani kama raia wa kawaida

Mama Kikwete apewa tuzo ya MDGs nchini Marekani

$
0
0

 

IMG_7012Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Millenium Development Goals, Women Progress Awards,2013, kutoka kwa Ms Jennie Yeung , Rais wa Shirika la Sun Zhong Shan Foundation lililo chini ya United Nations Education, Science, Cultural and Health Advancement  Foundation la nchini Marekani.  Mama Salma alipokea tuzo hiyo baada ya kutimiza baadhi ya malengo ya Millenia katika masuala ya ukimwi, elimu kwa watoto waliokosa fursa  na kuwawezesha wanawake kiuchumi nchini Tanzania. Kulia ni Katibu wa WAMA, Ndugu Daud Nassib na kushoto ni Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani.PICHA NA JOHN LUKUWI-MAELEZO

…………………………………………………………………….
Na Anna Nkinda – New York
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya Malengo ya Maendeleo ya Milinia ya mwaka 2013 kwa wanawake na Shirika la Voices of African Mothers (VAM) la nchini Marekani kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya kusaidia jamii wakiwemo wanawake na watoto.
Sherehe ya kukabidhi tuzo hizo zimefanyika  jana katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya  Umoja wa Mataifa  (UN) mjini New York.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) amekabidiwa tuzo hiyo kutokana na uongozi wake madhubuti, mafanikio na mchango wake na kujitoa kwake kuwasaidia wanawake na watoto wa Tanzania.
Akikabidhi tuzo hizo Nana – Fosu Randall ambaye ni Rais na mwanzilishi wa shirika hilo alisema kuwa tathimini ilitofanyika  kwa mwaka 2012 juu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia wametambua kwamba malengo matatu yamefikiwa nchini Tanzania   kabla ya muda uliowekwa wa kikomo wa mwaka 2015.
Alisema kuwa wake wa Marais wa Afrika wanamajukumu mbalimbali katika nchi zao ili kufikia Malengo hayo, Taasisi ya VAM imekuwa ikifanya tathimini juu ya hatua zilizofikiwa na Taasisi za wake wa Marais kupitia taarifa za mwaka na zingine zinazowasilishwa.
“Wanawake hawa wanastahili kutuzwa  kwani wamefanya kazi kubwa pamoja na kufanya shughuli zao katika mazingira yenye changamoto nyingi ukilinganisha na wenzao katika nchi zingine.
Hafla ya tuzo hizi siyo tu inasherehekea mafanikio ya wake wa marais wa Afrika bali pia inawahamasisha na kuwatia moyo wakati huu ambapo mwaka 2015 unakaribia”, alisema .
Alimalizia kwa kusema kuwa mara nyingi vyombo vya habari vimekuwa vikiandika habari  zisizokuwa sahihi kutokana na kazi zinazofanywa na wake wa marais lakini vinasahau kuandika mambo mazuri na kazi kubwa wanayoifanya ya kuwasaidia wananchi na kuviomba vyombo hivyo kubadilika na kuthamini kazi kubwa  wanayoifanya.
Akiongea mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Mama Kikwete alishukuru kwa tuzo aliyopewa na kusema kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimepiga hatua kubwa sana katika kufikia malengo ya milinia kwani vifo vya watoto vimepungua kwa asilimia 45 na 49 kwa watoto wachanga.
Alisema kuwa haya ni mafanikio makubwa sana japokuwa lengo ni kuondoa kabisa vifo ambavyo vinatokana na sababu ambazo zinazuilika  na katika malengo mengine maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) yanaendelea kupungua kutoka asilimia 5.7 kwa mwaka 2004 hadi asilimia 5.1 kwa mwaka 2011.
Mama Kikwete alisema, “Elimu ya msingi inatolewa bure kwa watoto wote walio na umri unaostahili na hatua kubwa imepigwa katika kupunguza ugonjwa wa maralia na vifo vya akina mama vinavyotokana na tatizo la uzazi”
Kwa upande wa harakati za kumkomboa mtoto wa kike alisema kuwa ni lazima ziendelee na zizingatie changamoto mpya za mazingira mapya kwani unapompatia elimu unampunguzia changamoto za ujinsia na kumpatia huduma ya afya ikiwemo uzazi wa mpango, unamuwezesha kushiriki zaidi shughuli za maendeleo ya kiuchumi, unasaidia familia yake na jamii kuweza kuendelea.
Kwa upande wake Dk. Judy Kuriansky ambaye ni mwakilishi wa Asasi zisizo za Kiserikali zilizo chini ya UN alisema kuwa wake wa marais wanafanya kazi kubwa ya kuisaidia jamii hivyo basi ni jukumu la kila mmoja kuwaunga mkono na kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kutimiza malengo ya maendeleo ya milinia.
Dk. Kuriansky alisema kuwa ili kufikia malengo ya milinia inatakiwa kuimarisha miundombinu iliyopo jambo ambalo litasababisha kuifikia jamii kwa ukaribu zaidi na kuweza kutatua changamoto zinazowakabili.
Tuzo hizo zimetolewa kwa mara ya kwanza na shirika hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya The reed for Hope (RFHF) na Bethesda Counsel kwa wake wa marais wa Afrika akiwemo Mke wa Rais wa Burundi Mama Dk. Denice Nkurunziza, Mke wa Rais wa Equatorial Guinea Mama Mintou Doucoure  Epse Traore  na Mke wa Rais wa Mali Mama Dk. Malika Issoufou.

DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MADAKTARI WA KICHINA IKULU

$
0
0

 

IMG_2109Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Madakatari wa Kichina waliofika IKulu Mjini Zanzibar, kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wao wa kazi,ambapo walikuwa wakishirikiana na Madakatari wazalendo katika kutoa huduma mbali mbali kwa wagojwa katika Hospitali za Unguja na Pemba.IMG_2115Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Madakatari wa Kichina waliofika IKulu Mjini Zanzibar, kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wao wa kazi, ambapo walikuwa wakishirikiana na Madakatari wazalendo katika kutoa huduma mbali mbali kwa wagojwa katika Hospitali za Unguja na Pemba.
IMG_2145Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapunduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Madakatari wa Kichina waliofika IKulu Mjini Zanzibar, kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wao wa kazi,ambapo walikuwa wakishirikiana na Madakatari wazalendo katika kutoa huduma mbali mbali kwa wagojwa katika Hospitali za Unguja na Pemba.{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

TAARIFA ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA KANDANDA TANZANIA TFF

$
0
0

 



tff_LOGOMAKOCHA STARS, IVORY COAST ANA KWA ANA
Wakati timu ya Ivory Coast imewasili nchini jana usiku (Juni 13 mwaka huu) kwa ndege maalum, kocha wa timu hiyo Sabri Lamouchi na mwenzake wa Taifa Stars, Kim Poulsen watakutana na waandishi wa habari kuzungumzia mechi yao.
 
Mkutano huo utafanyika kesho (Juni 15 mwaka huu) saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Mkutano huo pia utajumuisha makocha wa timu zote mbili. Ivory Coast inafanya mazoezi yake ya kwanza leo (Juni 14 mwaka huu) saa 9 alasiri kwenye viwanja vya Gymkhana.
 
Timu zote kesho (Juni 15 mwaka huu) zitafanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ivory Coast watafanya mazoezi saa 9 kabla ya kuwapisha Stars saa 10 kamili. Maandalizi yanaendelea vizuri ikiwemo kuwasili kwa maofisa wote wa mechi itakayochezwa Jumapili saa 9 kamili alasiri.
 
Wakati huo huo, mauzo ya tiketi kwa ajili ya mechi hiyo yameanza leo mchana (Juni 14 mwaka huu) katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, City Sports Lounge iliyoko Mtaa wa Samora na Azikiwe, Dar Live Mbagala, BMM Salon iliyoko Sinza Madukani na Uwanja wa Taifa.
 
Mauzo yataendelea kesho katika vituo hivyo, wakati siku ya mchezo yatafanyika Uwanja wa Taifa. Viingilio katika mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika katika kundi C ni sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 VIP B na VIP A sh. 30,000. Pia kuna kadi maalumu 100 kwa viti vya Wageni Maalumu (VVIP) zinazopatikana kwa sh. 50,000 katika ofisi za TFF.
 
TFF YATOA NOTISI YA MKUTANO MKUU
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ametoa notisi kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Shirikisho utakaofanyika Julai 13 mwaka huu kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam ukiwa na ajenda moja ya marekebisho ya Katiba.

 
Notisi hiyo imetolewa juzi (Juni 12 mwaka huu). Rais ameitisha Mkutano huo kwa mujibu wa Ibara ya 25(1) ya Katiba ya TFF baada ya kupata maagizo kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa barua yake ya Aprili 29 mwaka huu.
 
Ajenda rasmi na taarifa nyingine zitatumwa kwa wajumbe siku 15 kabla ya Mkutano huo kwa mujibu wa Ibara ya 25(4) ya Katiba ya TFF. Wanachama wa TFF ambao ni vyama vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu wanatakiwa kutuma majina ya wajumbe halali.
 
TFF inapenda kuwakumbusha wanachama wake kutuma majina ya wajumbe halali ili kufanikisha maandalizi ya Mkutano huo. Ni vizuri kuhakikisha kuwa jina linalotumwa ni la mjumbe halali wa Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya TFF.
 
RCL YAINGIA HATUA YA TATU WIKIENDI HII
Mechi za kwanza za hatua ya tatu ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao zinachezwa wikiendi hii kwenye viwanja vinne tofauti.
 
Mechi za kesho (Jumamosi) ni kati ya Kariakoo ya Lindi na Friends Rangers ya Dar es Salaam utakaochezwa katika Uwanja wa Ilulu mjini Lindi wakati Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Kimondo SC na Njombe Mji.
 
Timu za Machava FC ya Kilimanjaro na Stand United FC ya Shinyanga, Polisi Jamii ya Mara na Katavi Warriors ya Katavi zilizokuwa zipambane kesho mechi zao zimesogezwa mbele hadi keshokutwa (Jumapili). Mechi hizo zimesogezwa kutokana na viwanja vya Ushirika mjini Moshi na Karume mjini Musoma kuwa na shughuli nyingine za kijamii.
 
Hata hivyo, TFF imesisitiza kuwa ikibainika kuwa viwanja hivyo havikutumika kwa shughuli za kijamii siku hiyo ya Jumamosi, hatua kali zitachukuliwa kwa wanachama wake (vyama vya mpira wa miguu vya mikoa husika).
 
Mechi za marudiano za hatua hiyo ya tatu zitachezwa Juni 19 mwaka huu. Hatua ya nne ya RCL itachezwa kati ya Juni 23 na 23 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 29 na 30 mwaka huu.
 
 
 
RAMBIRAMBI MSIBA WA ABDALLAH MSAMBA
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Pan Africans, Simba na Taifa Stars, Abdallah Msamba kilichotokea juzi usiku (Juni 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
 
Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Msamba akiwa mchezaji, na baadaye kocha wa timu kadhaa alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea na kufundisha ikiwemo Villa Squad, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
 
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Msamba, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA) na klabu ya Villa Squad na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
 
Maziko ya mchezaji huyo yamefanyika leo (Juni 14 mwaka huu) katika makaburi ya Ndugumbi mkoani Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji wakiwemo wachezaji wa zamani na viongozi mpira wa miguu nchini. Mungu aiweke roho ya marehemu Msamba mahali pema peponi. Amina

RAIS WA ZANZIBAR DK ALI MOHD SHEIN AFUNGUA TAMASHA LA URITHI WA UTAMADUNI LA WATU WA MANGAPWANI ZANZIBAR

$
0
0

 


DSC_0509
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akiangalia Sabuni iliotengenezwa kwa Mwani katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi  wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja.DSC_0537
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wakwanza kulia akikaribishwa kwa ngoma ya Ndege mara alipowasili katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi  wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja.DSC_0541
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wakwanza kulia akiangalia Ngoma inayochezwa na Watoto  mara alipowasili katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi  wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja.
DSC_0559
Rais wa Zaanzibar Dk Ali Mohd Shein katikati akiangalia mchezo wa Bao la kete baada ya kuwasili katika Ufunguzi wa Tamasha la Urithi  wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja.kulia yake ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi na kushoto yake ni Mwenyekiti wa Tamasha hilo Mwinyi Jamal Ramadhan.

DSC_0574
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akiangalia Picha zilizochorwa kwa Ustadi pamoja na mazulia katika moja ya mabanda yaliokuwepo  katika  Ufunguzi wa Tamasha la Urithi  wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja.DSC_0604
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akichangia Upatu wa Maridadi ambao hutolewa baada ya Mwana kuolewa na watu kunywa chai(Kombela Bwana Harusi) katika  Ufunguzi wa Tamasha la Urithi  wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja.DSC_0619
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba ya makaribisho katika  Ufunguzi wa Tamasha la Urithi  wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja.kushoto yake ni Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk.DSC_0630
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Tamasha la Urithi  wa kiutamaduni wa watu wa Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja.
DSC_0655
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akisalimiana na Mzee Issa Suleiman Issa katika nyumba ya kiasili iliojengwa kwa makuti ya Kumba ikiwa ni ishara ya Ufunguzi wa Tamasha la Urithi la watu wa Mangapwani  Mkoa wa Kaskazini Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja.
 PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Nini tunajifunza kutokana na kuliki kwa taarifa za NSA toka kwa Edward Snowden?

$
0
0

 


Katika habari zilizotawala uwanja wa Tehama kwa wiki hizi ni habari ya Snowden, mfanyakazi wa shirika la usalama la marekani (NSA) pia ni muajiriwa wa zamani wa CIA aliyelikisha taarifa za siri zinazoelezea jinsi marekani inavyofuatilia taarifa za watumia mtandao bila idhini yao. Kuna wanaomuona Snowden kama hero na wengine wanamuona kama msaliti. Kulingana na maelezo ya Snowden kama alivyonukuliwa na mtandao wa Guarnian, inamaana kila unachoongea, unachotuma kinachunguzwa, wanafanya hivi kila mahali hadi kwa washika dau wakuu kwenye hii nyanja ambao ni Facebook na Google. Taarifa inaelezea kuwa, mashirika haya yametakiwa kuwapa NSA uwezo wa kuingia kwenye mitambo yao na kuchota chochote wanachotaka bila taarifa ya ziada.
 
Snowden ameamua kutoa taarifa hizi kwa kile alichokiita ni kuingiliwa kwa uhuru na unafasi wa watu (Privacy). Katika maelezo yake, Snowden anasema, taarifa nyingi zinazochunguzwa ni za watu na sio mashine hivyo watu hawa hawapo huru tena. Hii inakuja wakati serikali ya marekani ipo katika mvutano mkubwa wa masuala ya uvamizi wa mtandaoni na serikali ya China.
 
Siku chache zilizopita niliwahi kupata nafasi ya kuzungumza na professor mmoja anayejihusisha sana na mambo ya tafiti za mitandao hapa China, tulizungumza mengi, ila moja ya topiki ya mazungumzo ilikuwa ni kuhusu sababu za China kuzuia na kuendelea kuzuia mitandao mikubwa kama Google, Facebook, Twitter nk. Yeye alisema, sio tu kuwapa nafasi wataalamu wa nyumbani toka ushindani wa mataifa makubwa kama marekani bali pia hakuna kuaminiana kati ya nchi hizi mbili. Ukweli ni kuwa, kuna mambo mengi sana yanayoendelea nyuma ya panzia.

Aliongelea mambo mengi, pia akanigusia suala la vikwazo kwa Huawei, malalamiko ya marekani kufanyiwa uspy na China nk. Hivyo, kitu kimoja nilichojifunza hapa ni kuwa, jamaa wanajuana na ndio maana hawaaminiani. Nilipomuuliza je kuna sababu nyingine yoyote, alijibu, "Ken ding ya" akimaanisha haswaa. Sababu nyingine aliyoelezea ni kuwa ni jambo la hatari endapo nchi haitokuwa na umiliki wa taarifa muhimu za watu wake, hivyo kitendo cha kuruhusu makampuni ya kichina kuwa na vitu vya inawasaidia kuwa na jeuri na uwezo wa kulinda vitu vyao.  Hii ilinifanya nikumbuke lile vuguvugu la mapinduzi ya nchi za warabu (haswaa Tunisia) lilihamasishwa sana ndani ya Facebook.
Wakati ninatafakari na kutafuta baadhi ya reference kwa ajili ya makala hii, nikasema niende Facebook (ingawa ninajua kuwa ninafuatiliwa, hehe) ili nipate baadhi ya taarifa, nikakutana na picha kwenye ukurasa wa Masanja Mkandamizaji juu ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na JKT, kwakuwa mimi ni mmoja wa wapenzi namba moja wa JKT, nikasema ni ngoja nikasome majina ya hawa vijana, nilipofika kule, nikakutana na ujumbe mzito " Bandwidth Limit Exceeded". Hii ikanipa mwanga zaidi wa kufikiria katika mtazamo mwingine.

MWANANCHI

KUELEKEA MECHI YA STARS V IVORY COAST:KILIMANJARO LAGER YATAKA WATANZANIA WASIKATE TAMAA

$
0
0



Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inayodhamini Timu ya Taifa (Taifa Stars) akisalimiana na mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu wakati wa hafla fupi ya kuzungumza na wachezaji jana kabla ya mechi dhidi ya Ivory Coast. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki.
 
**********
Na Mwandishi wetu
Wadhamini wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Kilimanjaro Premium Lager wamewaomba watanzania washikane na kuungana pamoja wakati wa mechi dhidi ya Ivory Coast kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia kwani kuna watanzania ambao tayari wamekata tamaa.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (pichani)alisema Taifa Stars inatakiwa kuungwa mkono na kushangiliwa kwa nguvu kwani wachezaji wameonesha kuwa wana uwezo.
“Hawa ni wanajeshi wetu…nawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi…tuwape sapoti na tuoneshe uzalendo kwani kwenye mpira lolote linawezekana,” alisema.
Bw Kavishe alisema watanzania lazima welewa timu hii bado ni changa na ina wachezaji wapya wenye umri mdogo ambao wameonesha uwezo mkubwa.
“Hata ikitokea tusifuzu kwenda Kombe la Dunia, vijana wameshaonesha dalili nzuri na tuna imani tutafanya vizuri katika mashindano mengine kama AFCON na CHAN,” alisema.
Aliwataka wachezaji kutulia uwanjani na kutobabaishwa na ukubwa wa timu ya Ivory Coast kwani wana uwezo wa kuwafunga na kushangaza dunia nzima Jumapili.
“Hii ni kama fainali kwa Ivory Coast na wao pia wamebabaika na kuitilia maanani kabisa mechi hii kwa sababu tukiwafunga ina maana hawatakuwa na uhakika wa kufuzu katika hatua inayofuata,” alisema Kavishe.
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imetimiza mwaka mmoja tangu ianze kuidhamini Taifa Stars na wadau mbalimbali wamesifia udhamini huu kwani umeleta mabadiliko makubwa katika timu ya Taifa.
Timu ya Ivory Coast iliwasili nchini Alhamisi usiku na imeweka kambi katika hoteli ya Bahari Beach, Kunduchi tayari kwa mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Taifa JUmapili hii saa tisa kamili.
Kwa mujibu wa TFF maandalizi yote yamekamilika na mechi hii inatarajiwa kuangaliwa na maelfu ya watanzania watakaojitokeza uwanjani na kupitia runinga pia.
Ivory Coast inaongoza katika kundi C ikiwa na pointi 10, Tanzania ya tatu na pointi 6, Morocco ya tatu na pointi 5 na Gambia ni ya nne na pointi 1.
Viewing all 16721 articles
Browse latest View live


Latest Images